Cnaphalocrocis medinalis
Mdudu
Pia huitwa mkunja majani, nondo waliokomaa wana urefu wa ukucha wako na wana mistari ya kahawia ya zig-zag kwenye mbawa. Mayai kawaida huwekwa kwenye ncha ya jani. Viwavi hukunja jani la mpunga kuwazunguka na kuunganisha kingo za jani kwa nyuzi za hariri. Kisha hula ndani ya jani lililokunjwa lenye uwazi na kutengeneza michirizi ya wima myeupe angavu kwenye ubapa wa jani. Wakati mwingine, majani yanakunjwa kutoka ncha hadi sehemu ya kitako. Uwepo wa mayai yenye umbo la kisahani yaliyotagwa moja moja au ya mabaki ya kinyesi pia ni ishara za maambukizi.
Matoleo matano hadi sita ya vidusia vya mayai Trichogramma chilonis (wadudu waliokomaa 100,000 kwa hekta) kuanzia siku 15 baada ya kupanda ni bora na ni nafuu. Pia ulinzi wa maadui wa asili, kama buibui, mende wawindaji, vyura na kereng`ende. Kuvu au bakteria wa vimelea na pia baadhi ya virusi hutoa udhibiti mzuri wa idadi ya wadudu. Usambazaji wa majani ya mwarobaini shambani huwazuia wadudu waliokomaa kutaga mayai.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Ikiwa mashambulizi ni ya juu (>50%) wakati wa hatua ya kuchanua, nyunyiza flubendiamide @ 0.1ml au chlorantraniliprole @ 0.3ml/l ya maji. Viua wadudu vingine vyenye chlorpyriphos, chlorantraniliprole, indoxacarb, azadirachtin, gamma- au lamda-cyhalothrin pia husaidia, haswa ikiwa shambulio ni kali. Dawa zingine za kuua wadudu ni pamoja na alpha-cypermethrin, abamectin 2% kuua lava. Uangalifu uchukuliwe ili usitumie kemikali zinazosababisha mdudu kuzinduka/kufufuka.
Wadudu wanao sokota majani ya mpunga hutokea katika mazingira yote ya mpunga na huwa wengi zaidi wakati wa misimu wa mvua. Unyevu mwingi, maeneo yenye kivuli shambani, na kuwepo kwa magugu jamii ya nyasi kwenye mashamba ya mpunga na mipaka ya jirani hupelekea maendeleo ya wadudu. Maeneo ya mpunga yaliyopanuliwa yenye mifumo ya umwagiliaji, upandaji wa mazao mengi ya mpunga na ufufuaji unaosababishwa na viua wadudu ni mambo muhimu katika wingi wa wadudu. Matumizi makubwawa ya mbolea huchochea kuzaliana kwa haraka kwa wadudu. Katika maeneo ya kitropiki ya mpunga, wanakuwa amilifu mwaka mzima, ambapo katika nchi zenye hali ya hewa ya joto wanakuwa amilifu kuanzia Mei hadi Oktoba. Joto bora na unyevu ni 25-29 ° C na 80%, kwa mtiririko huo. Mimea michanga na ya kijani ya mpunga hushambuliwa zaidi.