Nilaparvata lugens
Mdudu
Tunutu na wadudu waliokomaa hukimbilia chini ya mmea na kunyonya maji kutoka kwenye shina na majani. Mimea hunyauka na kuanza kuwa njano. Msongamano mkubwa wa wadudu unaweza kusababisha majani kuanza kugeuka rangi ya machungwa-njano, kisha kuwa kahawia na makavu (hopper burn), na hatimaye, mmea hukauka na kufa. Shambani, dalili huonekana kwanza kama mabaka madogo lakini yanaweza kukua haraka kadiri panzi-vidukari wa mimea wanavyoenea. Majike hutaga mayai kwenye shina na katikati ya majani, na kusababisha uharibifu zaidi. Uzalishaji wa asali husababisha ukuaji wa ukungu wa masizi. Mimea ina vishada/masuke madogo, punje chache zilizoiva, na uzito mdogo wa punje.
Matibabu ya kibaolojia yanaweza kutumika katika msongamano mdogo wa idadi ya wadudu. Maadui wa asili wa panzi-vidukari wa kahawia ni pamoja na wadudu waeleaji maji(water striders), kunguni wa mirid, buibui, na nyigu na nzi wa vimelea vya mayai. Wadudu wanaweza kuzuiwa kwa mafuriko kwenye kitalu cha mbegu, kwa siku, ili tu ncha za miche zionekane juu (kuzamisha). Vinginevyo, vitalu vidogo vya mbegu vinaweza kufagiliwa kwa nyavu ili kunasa wadudu.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Dawa za kuua wadudu hupendekezwa tu ikiwa idadi muhimu hupatikana, au ikiwa panzi-vidukari wa kahawia ni zaidi kuliko maadui wa asili wanao onekana. Viua wadudu vinavyoweza kutumika dhidi ya wadudu ni pamoja na buprofezin, pymetrozine, etofenprox, au misombo mbadala. Epuka matumizi ya kemikali kama vile quinalphos, chlorpyriphos, au lambda-cyhalothrin au michanganyiko mingine ya parethroidi ya syntetisk ambayo inapelekea ukuaji wa ukinzani na kuibuka tena kwa wadudu.
Uharibifu husababishwa na Panzi-vidukari wa Kahawia waitwao Nilaparvata lugens. Wanaweza kuwa tatizo katika mazingira ya ardhi oevu yenye kulishwa na mvua na umwagiliaji, maeneo yenye hali ya chini ya maji shambani, kivuli kirefu, na unyevunyevu. Kivuli kilichofunga cha mimea ya mpunga, mazao yenye mbegu nyingi, matumizi mengi ya naitrojeni, na unyunyiziaji wa viuadudu wa msimu wa mapema (ambao huharibu maadui asilia) pia hupelekea maendeleo ya wadudu. Panzi-vidukari wa Kahawia huwa wengi zaidi wakati wa kiangazi kuliko msimu wa mvua. Wadudu wanaweza kufuatiliwa kwa kuinama juu ya mimea kidogo, na kuigonga polepole karibu na kitako, ili kuona ikiwa panzi-vidukari wa Kahawia wataanguka kwenye juu ya maji.