Dicladispa armigera
Mdudu
Mende walio komaa hula nje kwenye ngozi ya juu, na kusababisha muundo dhahiri wa michirizi myeupe, sambamba kwenye mhimili mkuu wa jani. Katika hali ya maambukizi makali, hata mishipa inaweza kuathiriwa, na kusababisha kuonekana kwa mabaka makubwa, meupe. Wadudu walio komaa mara nyingi huwa kwenye majani yaliyoharibiwa, kwa ujumla upande wa juu. Lava hula kwenye tishu za kijani kati ya ngozi mbili za juu za majani, huguguna kando ya mishipa na kusababisha mabaka meupe. Wanaweza kugunduliwa kwa kunyanyua jani lililoharibiwa kwenye mwanga au kwa kupitisha vidole kwenye vihandaki. Majani yaliyoshambuliwa hukauka, na kuleta mwonekano mweupe shambani. Kwa mbali, mashamba yaliyoharibiwa sana yanaonekana kama yamechomwa moto.
Udhibiti wa kibayolojia wa mdudu huyu bado unachunguzwa. Vimelea/vidusia wa lava, Eulophus femoralis, wameanzishwa nchini Bangladesh na India na huenda wakapunguza tatizo la hispa katika maeneo haya. Uhifadhi wa maadui asilia unaweza pia kuwa na jukumu muhimu katika udhibiti wa wadudu hawa. Kwa mfano, kuna nyigu wadogo ambao hushambulia mayai na lava na mdudu wa reduviid ambaye hula mende wakubwa. Pia kuna vimelea vitatu vya fangasi vinavyoshambulia wadudu walio komaa.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Katika hali ya shambulio kali, michanganyiko kadhaa ya kemikali iliyo na viambata vifuatavyo inaweza kutumika kudhibiti idadi ya wadudu: chlorpyriphos, malathion, cypermethrin, fenthoate.
Uharibifu husababishwa na wadudu walio komaa pamoja na lava wa hispa wa mpunga, Dicladispa armigera. Mende wakubwa hukwangua uso wa juu wa bapa za majani na kuacha safu ya chini tu. Mayai hutagwa ndani ya vitundo vidogo kwenye majani machanga, kwa ujumla karibu na ncha. Funza ni mweupe-njano na bapa. Hula ndani ya tishu za jani kwa kuchimba kwenye mhimili wa jani, na baadaye hujigeuza kuwa pupa ndani. Mende aliyekomaa ana umbo la mraba, karibu 3-5 mm kwa urefu na upana. Ana rangi ya buluu iliyokolea au nyeusi na miiba mwili mzima. Magugu ya nyasi, mbolea nyingi, mvua kubwa na unyevunyevu mwingi hupelekea shambulio la hispa wa mpunga.