Mahindi

Mbawakavu wa Matango

Diabrotica spp.

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Uharibifu wa ulaji kwenye mizizi na shina.
  • Hudhoofisha bua na kusababisha mmea kuanguka.
  • Mbawakawa wa rangi ya manjano-kijani wenye michirizi myeusi au madoa mgongoni.

Inaweza pia kupatikana kwenye

16 Mazao

Mahindi

Dalili

Wadudu waliokomaa hula hasa majani na maua, na hivyo kuingilia uchavushaji na ukuzaji wa nafaka/ganda/matunda. Lava hula nywele za mizizi, mizizi na shina, kupunguza uwezo wa mmea kunyonya maji na virutubisho kutoka kwenye udongo. Ncha za mizizi zinaweza kutafunwa hadi kwenye kitako cha shina la mmea au kuonekana kahawia na kutobolewa na kuwepo kwa vihandaki. Dalili huonyeshwa kama ukame au upungufu wa virutubisho. Katika hatua za baadaye za ukuaji wa mmea, uharibifu wa mzizi unaweza kudhoofisha shina na kusababisha shida ya kuvuna kwa sababu ya mmea kuanguka. Uharibifu wa lava pia huvutia viini vya magonjwa nyemelezi. Zaidi ya hayo, baadhi ya spishi za Diabrotica ni waenezaji wa virusi vya madoadoa ya njano ya mahindi na bakteria wanaosababisha mnyauko bakteria. Hii inaweza kusababisha hasara zaidi ya mavuno.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Aina kadhaa za nematodi, wadudu wanaowinda wadudu wengine (utitiri, wadudu) na nzi wa vimelea na nyigu wanaweza kutumika kudhibiti idadi ya mbawakavu. Kwa mfano, nzi wa tachinid Celatoria diabroticae wanaweza kuletwa wakati idadi ya mbawakavu wa tango sio kubwa sana. Kuvu Beauveria bassiana na Metarhizium anisopliae pia kwa kawaida hushambulia baadhi ya aina za Diabrotica.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Idadi ya uharibifu ya mbawakavu wa tango kawaida hutibiwa na dawa. Dawa za wadudu za kundi la acetamiprid au fendropathrin zinapaswa kutumika tu ikiwa mbawakavu watatokea kwa idadi kubwa, lakini zingatia masuala ya mazingira. Matibabu ya udongo na pyrethroids ni chaguo jingine.

Ni nini kilisababisha?

Spishi za Diabrotica ni kundi la wadudu waharibifu wanaoshambulia mazao kadhaa ya muhimu ya kilimo yakiwemo maharage na mahindi. Mbawakavu wa matango kawaida huwa na rangi ya manjano-kijani na hugawanywa katika vikundi viwili kulingana na vipengele vyao. Kundi la kwanza lina mistari mitatu myeusi chini ya mgongo, na la pili lina alama kumi na mbili nyeusi nyuma. Wadudu waliokomaa hujificha katika maeneo yanayowazunguka na huwa hai katikati ya masika, wakati halijoto inapoanza kupanda. Majike hutaga mayai katika makundi kwenye nyufa za udongo karibu na mimea inayowahifadhi. Lava hula ndani na juu ya mizizi kwanza, baadaye pia kwenye chipukizi huku wadudu wakubwa wakila majani, chavua na maua. Ukuaji kutoka yai hadi mdudu kamili huchukua karibu mwezi, kulingana na hali ya kimazingira. Wakati joto linaongezeka, mda wa ukuaji hupungua. Mbawakavu wa Matango wanapenda maeneo yenye unyevunyevu na usambazaji mzuri wa maji na hawapendi joto.


Hatua za Kuzuia

  • Kuchelewesha kupanda kunaweza kuzuia uharibifu mbaya zaidi.
  • Epuka kupanda mimea yako karibu na mimea mbadala kama vile matikiti, maboga au maharage.
  • Tumia matandazo kufunika udongo na kuvunja mzunguko wa maisha ya mbawakavu.
  • Tumia udongo wa kaolini kama utando wa kinga ili kuukinga mmea na mbawakavu.
  • Tumia mitego kufuatilia na kukamata wadudu kwa wingi.
  • Ondoa mabaki baada ya kuvuna na uyaharibu.
  • Panga mzunguko wa mazao na mimea isiyoshambuliwa.

Pakua Plantix