Muwa

Kipekecha shina wa Muwa

Diatraea saccharalis

Mdudu

Kwa Ufupi

  • "Tundu la sindano" uharibifu unaotokana na ulaji kwenye mashina.
  • Tishu za shina za ndani huliwa - ugonjwa wa "moyo uliokufa".
  • Mimea dhaifu na iliyodumaa.
  • Mimea iliyokomaa huanguka au kukatika.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Muwa

Dalili

"Tundu la sindano" uharibifu unaotokana na ulaji na utoboaji kwenye mashina unaosababishwa na lavau. Kwenye mimea michanga tishu za ndani ya shina huliwa, dalili inayoitwa moyo uliokufa. Kwenye mimea ya zamani, lava wachanga hujichimbia kwenye ala ya jani na kwapa. Kadiri lava wanavyokua, huanza kuchimba vihandaki kwenye shina. Mimea iliyoathiriwa sana huwa dhaifu na kudumaa na inaweza hatimaye kuvunjika au kuanguka wakati hali ya hewa si nzuri. Utoboaji hatimaye hupatikana kote kwenye mmea na kupunguza mavuno na ubora wa juisi.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Loweka miwa ya mbegu kwenye maji yenye joto la 25.6°C kwa angalau masaa 72 ili kuua 27-100% ya mayai ya kipekecha shina. Kuota hakuzuiliwi kufuatia matibabu haya, na miwa iliyoloweshwa huzalisha miwa mizuri zaidi. Idadi ya D. saccharalis inaweza kudhibitiwa na vimelea na wadudu wengi. Tumia chungu/majimoto, hasa majimoto wekundu Solenopsis invicta. Au tumia spishi za nyigu vidusia Trichogramma ili kupunguza idadi ya mayai.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Fuatilia mashamba kujua idadi kubwa ya wadudu inayoweza kusababisha uharibifu wa kiuchumi. Weka viua wadudu vyenye chlorantraniliprole, flubendiamide au vidhibiti vya ukuaji wa wadudu ili kuzuia lava wakubwa wasitoboe mashia.

Ni nini kilisababisha?

Joto huamua urefu wa mzunguko wa maisha. Ukuaji wa lava kawaida huhitaji siku 25 hadi 30 wakati wa hali ya hewa ya joto na takriban siku tano zaidi wakati wa hali ya hewa ya baridi. Mvua kubwa na joto la chini wakati wa majira ya baridi hupunguza idadi ya vipekecha shina wa miwa. Hali ya joto na mvua nyepesi hupendelea maisha na maendeleo ya wadudu. Kulima kwa kina kifupi huwezesha wadudu kusalia msimu mzima wa baridi katika uchafu wa mazao. Ukosefu wa wadudu wawindaji wa asili pia. Viwango vya juu vya mbolea ya naitrojeni vinaweza kusaidia maisha.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia aina zinazostahimili na sugu.
  • Epuka matumizi ya miwa ya mbegu iliyoharibiwa na kipekecha shina.
  • Ongeza silikoni kwenye udongo ili kupunguza uhai na majeraha ya vipekecha shina.
  • Choma miwa kabla ya kuvuna ili kupunguza idadi ya wadudu.
  • Haribu mara moja mabaki ya mazao shambani baada ya kuvuna kwa kuchoma, kulima au kuingiza maji shambani (mafuriko).

Pakua Plantix