Mzeituni

Ugonjwa wa Kigaga cha Tunda la Zeituni

Parlatoria oleae

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Wadudu wa msimu wa kwenye mimea jamii ya machungwa, ambao huacha makapi yanayotokana na ulaji wao kwenye mmea.
  • Matunda yaliyoshambuliwa hua na madoa ya zambarau ambayo yanawezekana kuonekana wakati wa mavuno.
  • Maambukizi makubwa yanaweza kusababisha kupukutika kwa majani mapema au ukosefu wa matunda kwa miaka kadhaa.

Inaweza pia kupatikana kwenye

6 Mazao
Mlozi
Tufaha
Aprikoti
Mzeituni
Zaidi

Mzeituni

Dalili

Kimsingi, sehemu zote za juu za mti husika zinaweza kushambuliwa na kigaga cha tunda la zeituni. Mara nyingi hupatikana kwenye gome la shina, matawi na vijiti. Ingawa, uwepo wake unaweza kuonyeshwa na madoa madogo meupe kwenye majani. Kwenye matunda ya zeituni, maambukizi husababisha uharibifu wa umbo la tunda na uwepo wa madoa meusi na kitovu cha kijivu karibu na eneo lililo liwa. Matunda mengine (matufaa na fyulisi, kwa mfano) yanaweza kuonyesha doa jekundu lenye weusi badala yake. Idadi kubwa ya wadudu husababisha kunyauka kwa majani, kubadilika rangi kuwa ya njano na kupukutika kwa majani. Kubadilika kwa rangi ya matunda, kudondoka kwa matunda kabla ya kukomaa, kudhoofika na kufa kwa vijitawi na matawi pia ni kawaida katika hali hizi.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Miongoni mwa nyigu wa vimelea(nyigu wanyoyaji), spishi kadhaa za Aphytis, Coccophagoides na Encarsia zinaweza kupunguza idadi ya wadudu wa kigaga cha tunda zeituni hadi nusu ikiwa zitaanzishwa dhidi ya kizazi cha majira ya kuchipua. Hakuna athari zinazo onekana kwa wadudu wa majira ya joto. Mdudu alae wadudu wengine aitwae Cheletogenes ornatus na spishi kadhaa za Chilorus wanaweza pia kuchukua jukumu muhimu katika kudidimiza idadi ya wadudu wa kigaga cha zeituni kwa kushambulia tunutu na wadudu wakubwa.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi yenye hatua za kinga na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Mafuta ya ukaa(dormant oils) yanaweza kunyunyiziwa kwenye sehemu za pingili(ngumu) za miti wakati wa msimu wa baridi. Katika msimu wa kuchipua, vidhibiti vya wadudu au viua wadudu vyenye organophosphates vinaweza kutumika wakati wa kuibuka kwa lava wanaotambaa katika msimu wa kuchipua. Ufuatiliaji ni muhimu ili kujua wakati sahihi wa kuweka dawa.

Ni nini kilisababisha?

Dalili husababishwa na ulaji wa wadudu wakubwa na tunutu wa mdudu wa kigaga cha tunda la zeituni aitwae Parlatoria oleae. Huonekana wakiwa wamejishikiza kwenye majani na matunda na pia kwenye gome la shina, vijitawi na matawi. Ukuaji wao ni wa haraka sana kiasi kwamba wanaweza kuunda tabaka kadhaa za wadudu hai kwenye tishu moja. Magamba yaliyokufa yanaweza kuwa juu yao na kuwalinda dhidi ya viuatilifu. Wanaweza kuwa na vizazi viwili au vitatu kwa mwaka kulingana na halijoto na mmea husika unaoshambuliwa. Kima cha chini cha ukuaji ni 10 ° C, lakini pia hudhurika na hali ya ukame. Madoa kwenye matunda husababishwa na udungaji wa sumu na hivyo ni ya kudumu, hata kama mdudu gamba akifa. Ugonjwa wa kigaga cha tunda la zeituni unaweza kuwa tatizo kubwa kwa matunda zeituni, hasa aina za mezani.


Hatua za Kuzuia

  • Angalia kanuni za karantini katika eneo au nchi yako.
  • Fuatilia bustani kwa ishara za uwepo wa kigaga cha tunda la mzeituni na kuona uibukaji wa lava watambaao.
  • Usafi wa mazingira ya bustani ni muhimu kwa uzalishaji wenye afya.
  • Tupa matunda yaliyoanguka, ambayo yanaweza kutumika kama hifadhi kwa majike ambao husalia kwa msimu mzima wa baridi.

Pakua Plantix