Mzeituni

Mbawakavu wa Gome la Mzeituni

Phloeotribus scarabaeoides

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Vitundu vya kuingilia kwenye gome la mti.
  • Vihandaki/njia za mkingamo za kupita chini ya gome.
  • Mguguno wa duara wa gome na kunyauka kwa vijiti na matawi.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao
Mzeituni

Mzeituni

Dalili

Majike waliokomaa hutoboa mashimo lukuki kupitia gamba la nje la gome na kuchimba kihandaki kinachokatiza kila upande kutokea kwenye sehemu ya kuingilia, moja kwa moja chini ya gome. Ndani ya kijitawi au tawi, jike hutaga hadi mayai 60 na lava wanapoanguliwa, huanza kutoboa nyama laini ya mti huo kwa kuelekea juu au chini. Hii inaonekana wazi wakati gome limekatwa na kuondolewa karibu na mashimo ya kuingilia. Ulaji huo husababisha kugugunwa kiasi aukabisa kwa sehemu ya kijitawi au tawi, kulidhoofisha kimuundo pamoja na kuharibu tishu za mishipa. Lava hujigeuza kuwa pupa ndani ya vijumba walimo kuwa wakila. Mbali na miti ya mizeituni, mbawakavu hawa hula oleander (Nerium oleander), mara chache hula miti ya mlangaria (Fraxinus excelsior) na mlisina(Syringa vulgaris).

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Mbawakavu huyu hushambuliwa na maelfu ya nyigu wa vimelea (wanyonyaji) wa familia kadhaa. Kuanzishwa kwa moja ya aina hizi na athari za udhibiti zinaweza kutofautiana mwaka hadi mwaka. Adui mkuu wa mbawakawa wa gome la mzeituni ni nyigu wa vimelea aina ya Cheiropachus quadrum, ambaye anaweza kupunguza idadi ya wadudu kwa 30-50%. Maadui wa asili wanaweza kuathiriwa vibaya na utumiaji wa viua wadudu vyenye pyrethroids.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Inashauriwa kuvutia mbawakavu kwa kutumia mitego ya harufu ya ethylene. Utumiaji wa viua wadudu vyenye pyrethroids kama deltamethrin umethibitishwa kupunguza kwa kiasi kikubwa idadi ya mbawakavu. Mbinu zote mbili zilitumiwa kama sehemu ya mbinu jumuishi pia zikaonyesha matokeo mazuri.

Ni nini kilisababisha?

Dalili husababishwa na mbawakavu wa gome la mzeituni, ambao wana vizazi 2 hadi 4 kwa mwaka, kulingana na hali ya mazingira. Majira ya kuchipua na mapema majira ya kiangazi huwa wanataga mayai kwenye matawi yaliyo pogolewa na kuni za miti a mizeituni zilizorundikwa badala ya miti hai. Lava ni xylophagous, kumaanisha kwamba hula kuni pekee. Mdudu huyo anaweza kuruka ndani ya eneo moja hadi mashamba mengine mapya. Wanaweza pia kubebwa kwa umbali mrefu wakati kuni zilizoshambuliwa au mimea hai ikisafirishwa. Maambukizi makubwa yanaweza kupunguza idadi ya maua na matunda ya mizeituni, na uharibifu unaoweza kufikia 70% ya mazao. Bustani za mizeituni zinaweza kushindwa kabisa kuzalisha ndani ya miaka 5 baada ya kushambuliwa. Miti michanga huathirika zaidi kwani uharibifu unaweza kulikata shina.


Hatua za Kuzuia

  • Matawi yaliyoshambuliwa yanapaswa kuondolewa na kuchomwa moto au kuzikwa chini kwa kina mbali na bustani.
  • Utaratibu huohuo unatakiwa kutumika kwa uchafu wa miti na matawi yaliyo pogolewa.
  • Fuatilia mizeituni kwa dalili za wadudu.
  • Kupungua kwa mavuno ya mizeituni kunaweza kutarajiwa endapo kuna vijumba zaidi ya 3 vya wadudu kwa kila mita ya tawi.
  • Hakikisha kwamba mimea mbadala inayoweza kuhifadhi mbawakavu wa gome la mzeituni haipatikani karibu na bustani.
  • Weka mbolea kwa uwiano mzuri ili kuongeza ukinzani wa asili wa mti kwa mbawakavu wa gome.

Pakua Plantix