Palpita vitrealis
Mdudu
Lava wachanga hula kwa kukwangua sehemu ya chini ya ngozi ya majani, na kuacha tabaka la juu likiwa sawa. Hii inasababisha mwonekano kama wa "vioo va dirisha", na ngozi ya juu iliyokauka, kahawia au kijivu. Lava wakubwa hula kwa kukata kiwambo kizima cha jani. Uharibifu huo unaweza kuenea hadi kwenye vikonyo na unawezakuasababisha kuanguka kwa majani. Mara nyingi pia huunganisha sehemu za jani au majani kadhaa pamoja kwa nyuzi za hariri ili kutengeneza viota, ambavyo baadaye watavitumia kwajili ya kujigeuza pupa. Punje nyeusi za vinyesi na nyuzi nyembamba za hariri zinaonekana wazi kwenye sehemu zilizoharibiwa za mmea. Ulaji pia unaweza kuonekana kwenye machipukizi ya katikati na kwenye matunda kwa namna ya mashimo ya ulaji au vijumba vinavyo enea hadi kwenye kiini.
Kuondolewa kwa maotea katika bustani kongwe za mizeituni ni njia bora ya kuzuia kuongezeka kwa haraka kwa nondo jasmine. Nyigu wa vimelea(wanyonyaji) wa spishi za Trichogramma na Apanteles na wadudu walao wadudu wengine wa spishi za Anthocoris nemoralis na Chrysoperla carnea ni maadui muhimu wa nondo jasmine. Matumizi ya vimiminika vyenye Bacillus thuringiensis pia yanapendekezwa dhidi ya P. unionalis.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Matibabu ya kemikali ya miti yanapaswa kuzingatiwa tu wakati zaidi ya 1% ya matunda yameathiriwa. Vitalu au mashamba mapya yanapaswa kutibiwa wakati zaidi ya 5% ya miti imeathiriwa katika msimu wa kuchipua. Viua wadudu vyenye viambato hai vya dimethoate, deltamethrin na cypermethrin vinaweza kutumika kwa udhibiti wa kemikali wa nondo jasmine katika bustani za mizeituni.
Dalili husababishwa na ulaji wa lava wa Palpita unionalis, ambao hushambulia hasa majani ya mizeituni. Nondo wana mwili wa kijani, karibu 15 mm kwa urefu, waliofunikwa kabisa na magamba meupe. Mabawa ni ya kung'aa, yenye uangavu kidogo na ukingo wenye pindo, mbawa za mbele zina madoa mawili meusi katikati na kingo za mbele za kahawia. Majike hutaga hadi mayai 600 kwenye majani machanga ya mizeituni, maua, matunda na matawi. Lava wanao anguliwa ni wa kijani-njano, takribani urefu wa 20 mm. Mwanzoni wana tabia ya umoja/kuwa pamoja, lakini baada ya muda hutawanyika na kutengeneza viota vyao wenyewe wakisuka pamoja majani kadhaa. Katika hali ya kawaida, viwavi si wengi wa kuweza kusababisha uharibifu mkubwa. Ingawa, wanaweza kuwa tatizo katika vitalu.