Mzeituni

Nondo wa Mzeituni

Prays oleae

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Michirizi/miguguno kwenye majani na kudondoka punje au vitu kuvuja kwenye upande wa chini wa majani.
  • Vipande vya majani vilivyo sokotwa pamoja na hariri.
  • Matunda hudondoka mapema kwani lava huingia na kula matunda kwa ndani.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao
Mzeituni

Mzeituni

Dalili

Dalili hutegemea sana majira ya mwaka. Kizazi cha kula majani hutoboa vihandaki kati ya safu mbili za ngozi ya majani na kuacha vishimo na chembechembe nyingi za kinyesi kwenye upande wa chini wa majani. Sehemu iliyo liwa mfano wa dirisha wakati mwingine huonekana. Kizazi kinacho kula maua hutengeneza kiota kwa kusokota pamoja maua kadhaa kwa nyuzi za hariri. Alama ya uwepo wa wadudu wanaokula huonyeshwa na punje nyingi za kinyesi. Katika kizazi cha kula matunda, lava hutoboa matunda madogo ya mzeituni mwanzoni mwa msimu wa joto na kutoka kwenye mzeituni mwanzoni mwa majira ya vuli, wakati wamekua kabisa, ili kujigeuza kuwa pupa kwenye udongo. Kudondoka kwa matunda mapema ni matokeo ya moja kwa moja ya uharibifu uliosababishwa na wadudu kwenye matunda.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Wadudu wanao kula wadudu wengine ni wengi na hujumuisha aina fulani za mchwa, krisopidi, na mbawakavu ambao hula mayai ya kizazi kimoja au kadhaa. Wadudu vimelea ni pamoja na aina kadhaa za nyigu, miongoni mwa wengine Trichogramma evanescens na Ageniaspis fuscicollis. Kimiminika chenye Bacillus thuringiensis kurstaki pia kimeonyesha kupunguza idadi ya nondo wa mzeituni kwa kiasi kikubwa. Mitego ya harufu ni mizuri sana katika kukamata nondo wakubwa na inapaswa kuwekwa mwanzoni mwa majira ya kuchipua.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Vizuizi vya kujamiiana au uwekaji wa ethilini unaweza kudhibiti wadudu kwa ufanisi. Msombo wa Organophosphates unaowekwa dhidi ya hatua ya lava wanao kula maua (kizazi cha kwanza) unaweza kutoa udhibiti mzuri.

Ni nini kilisababisha?

Uharibifu wa machipukizi, majani na matunda husababishwa na vizazi vitatu tofauti vya lava wa spishi ya Prays oleae. Nondo waliokomaa wana mbawa za mbele zenye rangi ya kijivu na matone ya kimetali ya fedha na madoa kadhaa meusi, ambayo katika baadhi ya sampuli yanaweza kukosekana. Mabawa ya nyuma ni ya kijivu sawia. Lava hutofautiana kwa rangi na ukubwa kulingana na kizazi kinachohusika. Kila moja ya vizazi hivyo huhusika katika sehemu maalum ya mzeituni. Lava wa kundi la kwanza (kizazi cha majani) huonekana katikati mwa majira ya kuchipua na kula ndani ya machipukizi na katika hatua ya baadaye, kwenye maua. Kundi la pili la lava (kizazi cha maua) hujitokeza mapema majira ya joto na ni waharibifu zaidi. Majike hutaga mayai kwenye tunda dogo karibu na shina, na lava wachanga huingia ndani ya zeituni na kula, na kusababisha kudondoka kwa matunda kwa kiasi kikubwa. Hatimaye, kizazi ambacho hutoka kwenye matunda huhamia kwenye majani, ambapo huchimba vihandaki kati ya safu za ngozi ya majani kama vile wadudu wachimba majani hufanya.


Hatua za Kuzuia

  • Angalia kanuni zinazowezekana za karantini katika nchi yako.
  • Panda aina sugu au zinazostahimili iwapo zinapatikana katika eneo lako.
  • Fuatilia miti ya mizeituni mara kwa mara kwa dalili za kushambuliwa na P.
  • oleae.
  • Tumia mitego ya harufu kujua idadi ya nondo waliopo.
  • Epuka matumizi ya viua wadudu vya wigo mpana ambavyo vinaweza kuua wadudu muhimu.
  • Usisafirishe sehemu yoyote ya mimea iliyoshambuliwa toka bustani moja hadi nyingine.

Pakua Plantix