Mzeituni

Ugonjwa wa Gamba Jeusi la Mzeituni

Saissetia oleae

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Utoaji wa asali/utomvu umande unaovutia chungu/sisimizi na kuvu wa masizi.
  • Majani yaliyoharibiwa huanguka mapema.
  • Ukuaji uliodumaa.
  • Mlundikano/uvimbe wa gamba jeusi kwenye sehemu ya chini ya majani na mashina.

Inaweza pia kupatikana kwenye

6 Mazao
Aprikoti
Mti wa jamii ya mchungwa
Kahawa
Mzeituni
Zaidi

Mzeituni

Dalili

Mdudu wa gamba jeusi hula kwa idadi kubwa kwenye majani na mashina na kunyonya maji maji mengi, na kusababisha kudhoofika kwa jumla kwa miti na kudumaa kwa ukuaji. Wakati wakila, hutoa utomvu mwingi wa asali unaoanguka na kufunika majani na matunda yaliyo karibu na weusi mwingi. Umande/utomvu wa asali unaweza kuvutia chungu na huvamiwa kwa haraka na kuvu wa masizi ambao hustawi kwenye utomvu wenye sukari, na hivyo kupunguza viwango vya usanisinuru kwenye majani. Majani yaliyoathiriwa vibaya yanaweza kuanguka mapema. Wadudu wakubwa huonekana kama uvimbe wa kijivu iliyokolea au kahawia-nyeusi kwenye sehemu za chini za jani na mashina.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Baadhi ya nyigu wanyonyaji, ikiwa ni pamoja na Scutellista caerulea, Diversinervus elegans na Metaphycus helvolus, pamoja na baadhi ya aina za wadudu kobe (Chilocorus bipustulatus) wanaweza kuangamiza idadi ya wadudu wa gamba jeusi katika mipangilio inayofaa. Ili kulinda maadui asilia wakazi, epuka kutumia viua wadudu vyenye wigo mpana katika mazingira. Mafuta ya canola au dawa za kuua wadudu za asili ya kuvu pia zinaweza kutumika kudhibiti kiwango wadudu wa gamba jeusi.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Tumia mitego ya kunata ya pande mbili, iliyosimamishwa kwenye dari(juu) ya miti, ili kutathmini uwepo wa wadudu wanaotambaa. Iwapo kiasi kitazidi, dawa za kunyunyuzia za narrow-ranged mineral white oil au kidhibiti cha ukuaji wa wadudu kiitwacho pyriproxyfen kinaweza kutumika. Dawa za kunyunyizia zenye chlorpyrifos pia zinaweza kutumika.

Ni nini kilisababisha?

Majike waliokomaa wa mdudu wa gamba jeusi wana kipenyo cha milimita 5 hivi na kahawia iliyokolea au nyeusi na mgongoni kuna kituta cha umbo la H mgongoni. Huhamia kwenye vijiti na matawi mwishoni mwa majira ya vuli na kubaki humo kwa maisha yao yote. Wadudu gamba wachanga (crawlers) ni wa manjano hadi rangi ya machungwa na hupatikana kwenye majani na matawi ya miti. Wanatawanyika kwa kutembea au wakati mwingine kwa kupeperushwa na upepo na kutua kando ya mishipa ya majani upande wa chini wa majani au kwenye vichipukizi vichanga. Wanastawi katika sehemu za miti zenye kivuli kikubwa, zisizopogolewa, hasa upande wa kaskazini. Kinyume chake, miti iliyo wazi, yenye hewa ya kutosha ni mara chache kuhifadhi idadi ya wadudu wa gamba jeusi. Wana kizazi kimoja au viwili kwa mwaka katika mazingira yasiyofaa, na kufikia viwili katika bustani zenye umwagiliaji. Mimea mbadala inayo hifadhi wadudu hawa ni pamoja na jamii ya machungwa, pistachio, peasi, miti jami ya mafyulisi(peaches & plum) na komamanga.


Hatua za Kuzuia

  • Fuatilia miti ya mizeituni mara kwa mara ili kugundua uvamizi wa ugonjwa wa gamba jeusi.
  • Kupogoa matawi vya kutosha kunaweza kuboresha mzunguko wa hewa na kuzuia mzunguko wa maisha ya mdudu wa gamba jeusi.
  • Katika hali ya uvamizi usio mkali, kuondoa kwa mikono kwa sehemu za mmea au kuponda ponda wadudu kunaweza kuwa na ufanisi.
  • Ondoa sehemu za miti zilizoshambuliwa na uzichome au uzike chini kwenye kina kirefu mbali na bustani.
  • Epuka matumizi ya kupita kiasi ya viua wadudu, kwani hii inaweza kuathiri vibaya idadi ya maadui asilia.
  • Simamia/linda mchwa kwa kuzungusha nyenzo nata kwenye mashina/pingili.
  • Pogoa vya kutosha ili kuzuia madaraja kati ya mimea.

Pakua Plantix