Mzeituni

Mdudu wa Mzeituni

Euphyllura olivina

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Wadu hao hula kwenye machipukizi, maua, mashina laini, na matunda madogo, kuharibu tishu.
  • Umande asali uliotolewa huvutia ukungu wa masizi na kuzuia usanisinuru (photosynthesis).
  • Utoaji wa nta husababisha ua na matunda madogo kuanguka.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao
Mzeituni

Mzeituni

Dalili

Wadudu wa mzeituni (psyllids) huathiri miti ya mizeituni kwa njia tatu: kwanza kwa njia ya kula moja kwa moja kwenye machipukizi, maua, mashina laini, na matunda madogo; pili, pia hutoa umande asali mwingi huku wakinyonya utomvu wa sukari wa tishu hizi, na hivyo kusababisha ukuaji wa ukungu wa masizi na kupunguza shughuli ya usanisinuru(photosynthesis) ya majani. Hatimaye, wakati wa mizeituni kutoa maua na kuweka matunda, tunutu kutoa nta husababisha udondokaji mapema wa maua na matunda madogo. Idadi kubwa ya wadudu inaweza kurudisha nyuma ukuaji wa miti michanga na kusababisha upotevu mkubwa wa mavuno. Miti iliyoshambuliwa sana inaweza kulea hasara ya 30% hadi 60% ya mavuno.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Wadudu walao wadudu wengine kama vile nyigu wa vimelea Psyllaephagus euphyllurae, kunguni haramia Anthocoris nemoralis, Chrysoperla carnea na mbawakavu mwekundu Coccinella septempunctata hupunguza idadi ya wadudu (psyllids) wa mzeituni. Kwa ujumla, hakikisha hauangamizi spishi hizi kwa kutumia viua wadudu vyenye wigo mpana (broad-spectrum). Viuwa wadudu visivyo na masalia na vya asili ambavyo vinafanya kazi dhidi ya wadudu hawa (psyllids) ni sabuni za kuua wadudu zenye mafuta ya mwarobaini na mafuta ya mbogamboga na matunda. Hizi zinapaswa kutumika kabla ya wadudu kutoa nta yao ya kinga. Sehemu zilizoshambuliwa zinaweza pia kukatwa ili kuimarisha mzunguko wa hewa kwenye matawi na majani na kuongeza ufichuaji wa wadudu (psyllids) wa mizeituni kwenye joto.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Unyunyuziaji wa viua wadudu kwa wakati mwafaka huwa na ufanisi dhidi ya wadudu hawa, lakini inapaswa kutumika tu kama suluhisho la mwisho. Bidhaa hizi zinapaswa kutumika kabla ya wadudu kutoa nta yao ya kinga ambayo inawapa ukinzani fulani dhidi ya dawa.

Ni nini kilisababisha?

Dalili husababishwa na ulaji ya wadudu (psyllids) wa mzeituni waitwao Euphyllura olivina. Wadudu wakubwa husalia msimu wote wa baridi katika sehemu zenye hifadhi katika shina la mizeituni. Wana mwili wenye rangi ya tan nyepesi, takriban 2.5 mm kwa urefu na mbawa za mbele na madoa machache meusi. Majike wanaweza kutaga mayai hadi 1000 kwenye mashina mapya na machipukizi wakati wa majira ya kuchipua. Tunutu ni bapa, kijani hadi hudhurungi, na hutoa utando mweupe wa nta unaowalinda. Katika halijoto kati ya 20° na 25°C, wanaweza kukamilisha mzunguko wao wa maisha kwa takriban miezi mitatu, na kuwa na hadi vizazi vitatu kwa mwaka katika hali hizi. Katika hali ya joto zaidi (zaidi ya 27 ° C), wadudu hawa (psyllids) huwa amilifu kwa kiasi kidogo sana na zaidi ya 32 ° C vifo vyao huongezeka. Ulaji wa tunutu na wadudu waliokomaa hupasuka tishu za mimea na kuharibu uwezo wa mimea kusambaza virutubisho kwenye sehemu zote. Hili huwa tatizo wakati wadudu (psyllids) wa mizeituni wakiwa kwenye maua, ambapo hatimaye huathiri uwekaji wa matunda na mavuno.


Hatua za Kuzuia

  • Fuatilia mimea mara kwa mara kujua idadi ya wadudu (psyllid) wa mizeituni, kuanzia mwanzoni mwa majira ya kuchipua.
  • Mitego ya kunata inapendekezwa kwajili ya kukamata wadudu hao (psyllids).
  • Hakikisha hauondoi wadudu walao wadudu wa mzeituni (psyllids) kwa kutumia viua wadudu vya wigo mpana.
  • Weka nafasi ya kutosha kati ya miti.
  • Hakikisha kuna mzunguko wa hewa ya kutosha kwenye majani pamoja na kufikiwa vizuri na mwanga wa jua, ili kutengeneza mazingira yasiyo rafiki kwa wadudu (psyllids).

Pakua Plantix