Mzeituni

Nzi wa Tunda la Mzeituni

Bactrocera oleae

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Matobo yenye umbo la pembetatu huonekana wazi kwenye matunda yanayo iva.
  • Kwanza huwa na rangi ya kijani lakini baadaye huwa na rangi ya manjano-kahawia.
  • Nyama ya matunda iliyoharibiwa kwa kuliwa lava/funza.
  • Matunda ya mizeituni yanaweza kukauka na kuanguka kabla ya kukomaa.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao
Mzeituni

Mzeituni

Dalili

Matundu ambayo majike hutaga mayai huonekana wazi kwenye matunda yanayo iva. Yana umbo la pembetatu na rangi ya kijani kibichi ambayo baadaye hugeuka manjano-kahawia. Ulaji wa lava/funza ndani ya matunda ndiyo husababisha uharibifu mbaya zaidi. Matunda ya mizeituni yanaweza kukauka na kuanguka mapema. Vidonda pia vinaweza kutumika kama sehemu za kuingilia kwa vimelea vya bakteria na fangasi. Mavuno na ubora wa matunda na mafuta huathirika.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Nyigu kadhaa wa vimelea wanaweza kuletwa katika bustani zilizoshambuliwa ili kudhibiti idadi ya inzi wa tunda la mzeituni. Opius concolor, Pnigalio mediterraneus, Fopius arisanus, Diachasmimorpha krassi au Eurytoma martellii ni baadhi ya hizo. Wadudu walao wadudu wengine ni pamoja na Lasioptera berlesiana. Dutu zitokanazo na mwarobaini au rotenone zinaweza kutumika kama dawa asilia. Poda ya Kaolin pia imetumiwa kwa mafanikio kuzuia majike kutaga mayai kwenye matunda. Matibabu ya kuzuia na dawa za zenye shaba (mchanganyiko wa Bordeaux, hidroksidi ya shaba, oxychloride ya shaba) pia hufanya kazi.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na hatua za kibiyolojia ikiwa zinapatikana. Viua wadudu vyenye viambata vya dimethoate, deltamethrin, phosmet au imidachlorid vinaweza kutumika wakati kiwango cha juu cha idadi ya wadudu kimefikiwa. Matibabu ya kuzuia na chambo za protini yenye sumu au mtego wa makundi pia yanawezekana.

Ni nini kilisababisha?

Dalili husababishwa na lava/funza wa nzi wa tunda la mzeituni aitwae Bactrocera oleae, ambae mwenyeji wake pekee ni mzeituni. Nzi wakubwa wana urefu wa 4-5mm, na mwili wenye rangi ya kahawia nyeusi, kichwa cha rangi ya machungwa na madoa meupe au ya manjano pande zote za kifua. Wana mbawa angavu na doa jeusi karibu na ncha na mishipa myeusi. Nzi wa mzeituni anaweza kuishi miezi kadhaa akiwa mkubwa. Majike wanaweza kutaga hadi mayai 400 maishani, kwa kutumia mwiba chini ya tumbo kutoboa ngozi ya matunda yanayoiva na kuweka yai moja ndani. Lava/funza wana rangi ya krimu nyeupe na hula nyama ya matunda, na kusababisha uharibifu mkubwa na hata kudondoka kabla ya kuiva. Inawezekana kuwepo kwa vizazi 2 hadi 5 vya nzi wa tunda la mzeituni kwa mwaka, kulingana na hali ya joto (nzuri zaidi ni 20-30 ° C).


Hatua za Kuzuia

  • Chagua aina sugu ikiwa zinapatikana.
  • Tumia mitego ya kunata au ya homoni za harufu ili kuwanasa nzi na kufuatilia idadi yao.
  • Vuna mapema ili kuepuka uharibifu mbaya zaidi, hasara katika mavuno inaweza kulipwa kwa faida katika ubora.
  • Usafi wa mazingira katika bustani ni muhimu ili kuzuia kuongezeka kwa idadi ya wadudu.
  • Safisha mti au ardhi ya matunda yaliyoambukizwa.

Pakua Plantix