Icerya purchasi
Mdudu
Wadudu kamili na tunutu hula kwa pamoja kwa kufyonza utomvu wa mmea na huzalisha kiasi kikubwa cha umande (majimaji) wa asali. Wanaweza kuonekana wakiwa wameyafunika mashina, majani, maua na machipukizi ya mimea inayoweza kuathirika na mdudu huyu. Kupungua kwa utomvu wa mimea kunaweza kusababisha kunyauka kwa majani na kukauka kwa matawi. Wadudu hawa wanapokula huzalisha umande mwingi wa asali unaofunika majani na kuchochea ukuaji wa ukungu mweusi wa masizi. Wakati wa mashambulizi mkubwa ya ugonjwa, kupukutika kwa majani na kukauka kwa matawi, pamoja na kupungua kwa viwango vya usanidimwanga, husababisha kupungua kwa uimara wa miti na kupungua kwa ubora na mavuno ya matunda.
Wadudu maarufu wanaowinda na kula Mdudu-gamba Takia-pamba ni pamoja na wadudu kibibi na mbawakimia. Maadui maalum wa asili ni pamoja na mbawakavu vedalia ambao lava wachanga wanakula mayai ya wadudu gamba hawa na mbawakavu vedalia wakubwa wanakula hatua zote za Mdudu-gamba Takia-pamba. Vidudu wa nzi wanaofahamika kitaalamu kama Cryptochaetum iceryae, pia ni vidudu vyenye ufanisi mzuri katika kudhibiti Mdudu-gamba Takia-pamba.
Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibaiolojia ikiwa yanapatikana. Wadudu-gamba kamili na tunutu watambaaji wanafunikwa na utando mnene wa nta, na hivyo kufanya tiba ya kemikali za kuua wadudu dhidi ya wadudu hawa kuwa ngumu. Ili kuwadhibiti inashauriwa kutumia kwa wakati muafaka dawa zinazotokana na kiambato hai cha acetamiprid. Kupulizia mafuta ya petroli mara baada ya kuanguliwa kwa mayai inaweza kuzuia wadudu wadogo wanaotambaa wasile tishu za mmea.
Dalili kwenye miti zinatokana na Mdudu-gamba aitwae Icerya purchasi kufyonza utomvu wa floemu. Katika maeneo mengine ya kijiografia, aina zingine za wadudu hawa zinaweza kuwa ndo zipo kwa wingi, kwa mfano vidung'ata (vidukari-sufu) wa michungwa. Wadudu-gamba Takia-pamba wana urefu wa takribani milimita 10–15 na wanaweza kukamilisha mzunguko wao wa maisha ndani ya muda wa miezi 2 wakati wa hali nzuri. Majike yanaweza kuzalisha mayai hadi 1000, ambayo hubebwa kwenye kifuko cha mayai yaliyo mithili ya pamba kwenye tumbo na kuyataga kwenye majani. Tunutu (wadudu wachanga wanaotambaa) wapya walioanguliwa huanza kwanza kula kwenye majani, na kwa kawaida kando ya mishipa ya jani, na matawi machanga. Kadri Wanapoendelea kukua, wanaweza pia kupatikana kwenye matawi na shina, na mara chache kwenye matunda. Wadudu hawa hupendelea hali ya unyevu na ubaridi, na hustawi vizuri kwenye miti ya machungwa yenye msongamano mzito wa paa la majani. Kadri wanavyoendelea wadudu hawa hujenga utando mnene wa nta ulio mithili ya pamba inayowalinda. Wadudu aina ya majimoto wanaokula kwenye umande wa asali huwalinda wadudu gamba na tunutu na hivyo kuvuruga shughuli za maadui wa asili wa wadudu hawa. Mimea aina za Mora, Acacia, na Rosmarinus ni mimea mbadala ambayo uhifadhi wadudu hawa, lakini mimea hii pia inaweza kuharibu aina nyingi za miti ya matunda na misitu, pamoja na vichaka vya mapambo.