Helicoverpa armigera
Mdudu
Lava hula sehemu zote za mmea, lakini wanapendelea maua na maganda. Mashimo ya ulaji huonekana kwenye maganda. Wakati mwingine lava/funza wanaweza kuonekana wakirandaranda nje ya maganda wakati wa kula. Ikiwa hakuna maua au maganda, lava wanaweza pia kula majani na machipukizi ambapo wanaweza kusababisha kudondoka kwa majani.
Jaribu kuweka idadi ya wadudu wenye manufaa wanaonyonya au kushambulia Helicoverpa ndani na nje ya shamba lako. Nyigu aina ya Trichogramma, Microplitis, Heteropelma, Netelia sp., wadudu wanaowinda wadudu wengine kama vile big-eyed bug, glossy shield bug na spined predatory shield bug huzuia ukuaji wake. Chungu na buibui hushambulia lava. Dawa za asili za kuua wadudu zenye NPV (Nucleopolyhedrovirus), Metarhizium anisopliae, Beauveria bassiana na Bacillus Thuringiensis pia zinaweza kutumika. Bidhaa za mimea, kama vile kizidu cha mwarobaini na pilipili au kitunguu saumu zinaweza kunyunyiziwa kwenye majani ili kudhibiti wadudu.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia. Fuatilia viwango vya idadi ya wadudu ili kujua umuhimu wa mbinu ya kikemikali. Kiwango sahihi cha kiuchumi kimewekwa kuwa nondo 8 kwa usiku @mitego 4/ekari katika siku tatu zinazofuata. Mdudu huyo amekuza kiwango fulani cha ukinzani dhidi ya dawa za kuua wadudu zenye pyrethroid.
Wadudu waliokomaa wana urefu wa cm 1.5 na wana mabawa ya karibu 4.0 cm. Mwili wao wa kijivu, hudhurungi una kifua chenye manyoya na mbawa za mbele za rangi ya hudhurungi ya kufifia zenye ukanda wa hudhurungi nyeusi uliojaa madoa meusi kwenye kingo. Mbawa za nyuma ni nyeupe zenye mstari wa rangi ya manjano na ukanda mpana mweusi wenye kiraka hafifu kwenye ukingo. Majike hutaga mayai meupe yenye umanjano kwenye mimea inayotoa maua au mimea inayokaribia kuchanua. Vipengele vya lava hutofautiana kulingana na hatua zao za ukuaji, lakini wote wana tumbo lenye rangi hafifu. Wanapokomaa, wao huota madoa meusi madogo na mistari miwili myeupe angavu au ya manjano kwenye ubavu wao. Muda wa hatua mbalimbali za maisha unahusishwa kwa karibu na hali za kimazingira, hasa joto na upatikanaji wa chakula.