Spodoptera litura
Mdudu
Uharibifu unaotokana na wadudu kula mimea huonekana wazi kwenye majani. Lava hukwangua tishu za jani, na kutengeneza mashimo makubwa yasiyo na umbo maalumu. Inaweza kusababisha mmea kupukutika majani kabisa. Maua na vitumba au maganda pia hushambuliwa na kuonyesha mashimo yalitokana na wadudu kula. Katika udongo mwepesi pia mizizi huharibika. Kutokana na ulaji mkubwa, ni vikonyo na matawi pekee ndivyo vinabaki.
Dawa za Kibaiyolojia za kuua wadudu (Bioinsecticides) zinazotokana na Nuclear Polyhedrosis Virus (NPV) au Bacillus thuringiensis zinaweza kutumika kwenye mayai na lava. Suluhisho la kutumia chambo zinazotokana na makapi ya mpunga, molasi au sukari guru zinaweza kusambazwa kwenye udongo wakati wa masaa ya jioni. Mafuta yaliyokamuliwa kutoka kwenye majani ya mwarobaini au mbegu za ngano na Pongamia glabra (mmea jamii ya mikunde), zina ufanisi wa juu dhidi ya viwavi aina ya Spodoptera litura. Kwa mfano, azadirachtin 1500 ppm (5 ml/l) au NSKE 5% inaweza kutumika wakati wa hatua ya mayai na hivyo kuzuia mayai yasianguliwe.
Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibaiyolojia ikiwa yanapatikana. Utumiaji mwingi wa viua wadudu unaweza kusababisha usugu kwa wadudu. Ili kudhibiti lava wachanga, aina kadhaa za dawa za kuua wadudu zinaweza kutumika, kwa mfano, dawa zinazotokana na chlorpyrifos, emamectin, flubendiamide, chlorantraniliprole, indoxacarb au bifenthrin. Ufumbuzi wa kutumia chambo pia hupunguza kwa ufanisi idadi ya lava wakubwa (mabuu).
Dalili husababishwa na mabuu ya Spodotpera litura. Nondo waliokomaa wana miili ya rangi ya kijivu-kahawia na mbawa za mbele zilizo na rangi tofauti na alama mithili ya mawimbi meupe kwenye kingo. Mbawa za nyuma zina mng'ao mweupe na mistari ya kahawia kando ya kingo na mishipa. Majike hutaga mamia ya mayai kwa makundi kwenye upande wa juu wa majani, yaliyofunikwa na magamba ya njano kahawia. Baada ya kuanguliwa, lava wa kijani iliyofifia na ambao hawana nywele hutawanyika haraka na kuanza kula majani kwa wingi. Lava wakubwa wana rangi ya kijani kibichi hadi kahawia na madoa meusi ubavuni na matumbo angavu. Mistari miwili ya longitudo (iliyo wima) yenye rangi ya njano hupita pembezoni, zikikatizwa na madoa meusi ya pembetatu. Mstari wa rangi ya chungwa hupita kwa nyuma katikati ya madoa haya. Lava hula wakati wa usiku na kukimbilia kwenye udongo wakati wa mchana. Lava na viwavi wakubwa hustawi katika halijoto kati ya 15°C na 35°C, kiwango cha juu zaidi cha 25°C. Unyevu wa chini na joto la juu au la chini hupunguza uzazi na kuongeza mzunguko wa maisha yao.