Chrysodeixis includens
Mdudu
Uharibifu hutokana na viwavi kula sehemu za mimea. Lava wachanga hula kwanza kwenye upande wa chini wa majani na kuacha sehemu ya juu, hivyo kusababisha sehemu wazi zilizoliwa zinazofanana na dirisha wakati mwingine hujulikana kama ‘dirisha la ulaji’. Lava wakubwa hula kwenye jani zima kutoka kwenye kingo zake, wakiepuka mishipa mikubwa ya ulalo, na kusababisha mashimo yasiyo na mpangilio na kingo zilizo chakazwa. Upukutishaji wa majani usio wa kawaida, ulaji kutoka sehemu ya chini ya mmea, ndani ya mwavuli/dari, na kuelekea juu na nje. Mara chache hushambulia maua au maganda. Hata hivyo, katika hali ya kupukutika kwa majani ya mmea, lava kwa kawaida wataendelea kula kwenye maganda ya soya.
Maadui asilia ni pamoja na nyigu vidusia wanaokula lava wa dengi wa soya: Copidosoma truncatellum, Campoletis sonorensis, Casinaria plusiae, Mesochorus discitergus na Microcharops bimaculata, Cotesia grenadensis na nzi wa vimelea Voria ruralis, Patelloa na spishi zingine kama vile Patehoro Lespesia. Bidhaa zenye Baculoviruses, Bacillus Thuringiensis au Spinosad pia zimetumika kudhibiti dengi wa soya.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Dengi wa soya pekee hawezi kuwa tishio kwa mazao. Zingatia uharibifu unaoletwa na wadudu wengine wanaoweza kupukutisha majani wakati wa kufanya uamuzi wa usimamizi. Matibabu yanapendekezwa ikiwa upukutishaji wa majani unafikia 40% kabla ya kuchanua, 20% wakati wa kuchanua na kujaza maganda, au 35% kutoka wakati wa kujaza maganda hadi kuvuna. Bidhaa zilizo na indoxacarb, methoxyfenozide au spinetoram zinaweza kutumika. Epuka viua wadudu vya familia ya pyrethroids kwani ukinzani/usugu wa bidhaa hizi umeelezewa.
Uharibifu husababishwa na lava wa dengi wa soya Pseudoplusia includens. Nondo waliokomaa wana rangi ya kahawia iliyokolea, mbawa za mbele zina rangi ya kahawia yenye madoadoa na kumetameta kwa shaba nyeusi hadi dhahabu. Alama mbili za fedha zinazovutia zinaonekana katikati yake. Nondo jike hutaga mayai kwenye upande wa chini wa majani, katika sehemu ya chini ya mmea na ndani ya mwavuli/dari. Lava wana rangi ya kijani kibichi na mistari myeupe kwenye ubavu na mgongoni. Wana sifa ya kuwa na jozi tatu za miguu maalum iliyogawanywa bila usawa sambamba na mwili (2 katikati ya mwili, moja kwenye mkia). Mpangilio huu husababisha lava kuinua mgongo wao wakati wa kutembea, na hivyo jina lao la kawaida 'Dengi'. Pupa husokota kifuko kwenye sehemu ya chini ya majani.