Mpunga

Viwavijeshi Vamizi

Spodoptera frugiperda

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Uharibifu unaotokana na kula kwenye sehemu zote za mmea.
  • Kinyesi kinaweza kuonekana kwenye majani.
  • Kiwavi ana alama kama Y kwenye paji la uso na vidoti vinne mgongoni.

Inaweza pia kupatikana kwenye

25 Mazao

Mpunga

Dalili

Lava wa kiwavi jeshi husababisha uharibifu kwa kula sehemu zote za mmea. Lava wachanga huanza kwa kula upande mmoja wa tishu za jani, na kuacha tabaka la upande wa pili likiwa halijaathiriwa ("ulaji wa dirisha"). Miche inaweza kuliwa hadi kuharibu machipukizi na sehemu za ukuaji. Lava wakubwa huacha safu maalum ya matobo na kingo zenye mipasuko kwenye majani, pamoja na mistari ya kinyesi cha lava. Pia wanaweza kukata sehemu ya chini ya mmea au kushambulia sehemu za uzazi za mmea au matunda machanga. Katika hali ya uvamizi mkubwa, viwavi jeshi wanaweza kusababisha upotevu mkubwa wa majani.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Nyigu vidusia wanaofaa kudhibiti viwawi na lava hawa ni pamoja na Cotesia marginiventris, Chelonus texanus, na C. remus. Nzi kidusia (nzi vimelea/wanaokula wadudu wengine) anayejulikana zaidi ni Archytas marmoratus. Wadudu wanaokula lava ni pamoja na mbawakawa wa ardhini, mdudu ajulikanae kama spined soldier, wadudu wa maua, ndege au panya. Dawa za kuua wadudu (Viuatilifu) za kibiolojia zenye mafuta ya mwarobaini, Bacillus Thuringiensis, au Baculovirus Spodoptera, pamoja na Spinosad au Azadirachtin zinaweza kupuliziwa. Katika mahindi, mchanga mwekundu, chumvi ya mawe, unga wa mkaa, au majivu ya nzi yaliyowekwa kwenye shina kuu yanazuia lava wa viwavi jeshi vamizi kula na kuwaua (ufanisi wa 100%, 98%, 90%, na 80%, mtawalia).

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu shirikishi zenye hatua za kinga pamoja na tiba za kibaiolojia ikiwa zinapatikana.Dawa za kuua wadudu zinavyopendekezwa ni pamoja na esfenvalerate, chlorpyrifos, na lambda-cyhalothrin. Wakulima pia wanashauriwa kutumia chambo chenye sumu kilichotengenezwa kwa kutumia dawa hizi za kuua wadudu ili kudhibiti lava wakubwa.

Ni nini kilisababisha?

Mayai hutagwa kwa makundi yenye mkusanyiko wa mayai 100-300 kwenye upande wa chini wa majani, na mara nyingi yakifunikwa na magamba. Lava wanakuwa na rangi ya kahawia hafifu au kijani hadi karibu na nyeusi, na wana mistari inayopita ubavuni na mstari wa manjano unaopita mgongoni. Nondo wana mbawa za nyuma ambazo ni nyeupe na angavu na mbawa za mbele za kahawia zenye madoa yenye alama zenye rangi nyepesi na nyeusi. Kila bawa la mbele lina doa jeupe linaloonekana karibu na nchakabisa. Virutubisho na joto hubainisha muda/urefu wa awamu mbalimbali za mzunguko wa maisha ya viwavi hawa. Majira ya kuchipua yenye ubaridi na maji maji, yakifuatiwa na hali ya hewa ya joto na unyevu, hustawisha mzunguko wa maisha wa mdudu huyu.


Hatua za Kuzuia

  • Panda mimea yenye ustahimilivu zaidi dhidi ya magonjwa.
  • Kagua uwepo wa nondo na wakamate kwa makundi kwa mwanga au kwa mitego ya harufu (mitego 10/ha).
  • Panda mapema ili kuepuka kipindi cha idadi ya juu ya wadudu.
  • Udhibiti wa magugu unashauriwa.
  • Vuna mapema ili kuepuka uharibifu wa kudumu.
  • Katua ardhi ili kuwaanika lava na pupa kwenye joto kali.

Pakua Plantix