Tuta Absoluta
Mdudu
Uvamizi hutokea wakati wowote katika mzunguko wa zao na unaweza kuathiri sehemu yoyote ya zao. Lava hupendelea machipukizi ya kwenye ncha za mmea, majani machanga laini, na maua. Kwenye majani, lava huchimba vihandaki visivyo na mpangilio, vya kijivu hadi vyeupe ambayo vinaweza baadaye kuwa na tishu zilizo kufa. Lava wanaweza kuchimba vishimo kwenye mashina ambavyo huathiri ukuaji wa mimea. Kwenye matunda, alama nyeusi zinaweza kupatikana kwenye sehemu ambazo lava huingilia au kutokea. Matundu hayo hutumika kama sehemu za kuingilia kwa vimelea vya upili, na kusababisha kuoza kwa matunda.
Wadudu kadhaa wanaokula T. absoluta wamepatikana: miongoni mwa spishi nyingi nyigu vidusia Trichogramma pretiosum, na mende Nesidiocoris tenuis na Macrolophus pygmaeus. Aina kadhaa za fangasi ikiwa ni pamoja na Metarhizium anisopliae na Beauveria bassiana hushambulia mayai, lava na nondo walio komaa. Viziduo vya mbegu za mwarobaini au viua wadudu vyenye Bacillus thuringiensis au Spinosad pia hufanya kazi.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Dawa zinazopendekezwa kwa ajili ya udhibiti wa wadudu wa tuta absoluta huenda zisifanikiwe kutokana na hali ya kujificha ya lava, uwezo mkubwa wa kuzaliana wa mdudu huyu na kukuza ukinzani dhidi ya madawa. Ili kuepuka ukinzani, tumia kwa mzunguko aina kadhaa za viua wadudu kama vile indoxacarb, abamectin, azadirachtin, fenoxycarbe+lufenuron.
Tuta absoluta ni wadudu waharibifu wa nyanya kwa sababu ya uwezo wake mkubwa wa kuzaliana, na hadi vizazi 12 kwa mwaka. Majike wanaweza hutaga hadi mayai 300 ya rangi ya krimu kwenye upande wa chini wa majani. Mayai huanguliwa kwa joto la 26-30ºC na unyeve wa anga 60-75%. Lva wana rangi ya kijani kilichopauka wakiwa na sifa ya mstari mweusi nyuma ya vichwa vyao. Chini ya hali nzuri (joto, unyevu), maendeleo yao yanakamilika kwa siku 20. Wadudu waliokomaa wana rangi ya kahawia ya fedha, urefu wa 5-7 mm na hujificha katikati ya majani wakati wa mchana. Tuta absoluta anaweza kusalia msimu wote wa baridi kali kama mayai, lava au mdudu kamili kwenye majani au kwenye udongo.