Nyingine

Mbawakavu wa Majani ya Nafaka

Oulema melanopus

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Michirizi myembamba, mirefu na myeupe kwenye sehemu ya juu ya jani.
  • Sehemu iliyoathiriwa inaweza kuonekana kuwa imemeguka na ya zamani.
  • Wadu wakubwa wana vifuniko vya mabawa vya bluu-nyeusi na kichwa na miguu myekundu.
  • Mayai hutagwa upande wa chini wa majani.

Inaweza pia kupatikana kwenye

4 Mazao

Nyingine

Dalili

Mbawakavu huyu huvutiwa zaidi na nafaka kama vile oti, shayiri, na rai/ngano nyekundu, lakini mmea anao upenda zaidi ni ngano. Pia ana aina mbadala za mimiea mwenyeji, kama vile mahindi, mtama, na nyasi. Lava hula kwenye ngozi ya juu ya majani na kusababisha uharibifu mkubwa wa mzunguko mzima wa maisha. Tabia yao ya ulaji ina sifa ya kuondolewa kwa tishu za majani hadi kwenye tabaka la chini la ngozi ya juu, na kuacha makovu membamba, marefu, meupe au michirizi ambayo inaweza kuwa mingi katika hali ya maambukizi. Hata hivyo, mbawakavu waliokomaa kwa kawaida huhamia mimea au mashamba mengine kadri wanavyo kula, kumaanisha kuwa uharibifu mkubwa kwenye shamba moja ni nadra. Kutoka mbali, shamba lililoathiriwa linaweza kuonekanalimechakaa na la zamani, lakini kwa kawaida uharibifu hauzidi 40% ya eneo lote. Mbawakavu anaweza kuwa wadudu waharibifu na wa kudumu katika baadhi ya maeneo yanayolima nafaka.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Baadhi ya spishi za sota/nematodi za jenasi ya Steinernema zimeonyesha kuwashambulia wadudu waliokoma ambao hujificha wakati wa baridi kwenye udongo, na kuwazuia kuzaliana katika majira ya kuchipua. Hata hivyo, ufanisi wao unaweza kutofautiana kulingana na joto. Baadhi ya wadudu kobe pia huwinda mayai na lava. Nzi aina ya tachinid Hyalomyodes triangulifer huwa vimelea wa mbawakavu waliokomaa na wanapatikana kibiashara ili kudhibiti idadi ya O. melanopus. Lava, kwa upande wake, wanaweza kudhibitiwa na nyigu vidusia wa Diaparsis, Lemophagus curtis, na Tetrastichus julis. Hatimaye nyigu Anaphes flavipes huharibu mayai na pia ni wakala mzuri wa kudhibiti.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi yenye hatua za kinga na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Dawa za kuua wadudu zenye viambato amilifu vya Gamma-cyhalothrin ndizo zenye ufanisi zaidi dhidi ya wadudu huwa kwa sababu huathiri mayai na lava. Unyunyiziaji unapaswa kufanywa wakati wadudu wakubwa wanataga mayai yao au wakati 50% ya mayai yameanguliwa. Matumizi mabaya yanaweza kuongeza idadi ya O. melanopus kwa sababu wadudu wanaokula wenzao wameuawa. Dawa zingine za wadudu za familia za organophosphates (malathion) na pyrethroids pia zimetumika dhidi ya O. melanopus.

Ni nini kilisababisha?

Uharibifu huo unasababishwa zaidi na mabuu ya mbawakavu Oulema melanopus. Wadu kamili wana urefu wa 5 mm na wana vifuniko vya mabawa vya bluu-nyeusi na kichwa na miguu myekundu. Wanaenea hadi nje ya shamba na hutumia wakati wao wa baridi katika maeneo yaliyohifadhiwa kama vile safu kukinga upepo, majani ya mimea, na nyufa za magome ya miti. Hujitokeza wakati hali ya mazingira inapokuwa rafiki wakati wa majira ya kuchipua, katika kiasi cha joto takribani 10 °C. Majira ya kuchipua yenye joto yanafaa kwa mzunguko wa maisha yake, wakati vipindi vya baridi huzuia. Baada ya kujamiiana, majike huanza kutaga mayai ya manjano angavu, yenye umbo la mche duara kwenye upande wa chini wa majani, mara nyingi kando ya mshipa wa katikati, na kuendelea kufanya hivyo kwa muda mrefu (siku 45-60). Lava huanguliwa baada ya siku 7-15 na kuanza kula juu ya ngozi ya juu ya majani, na kusababisha uharibifu mbaya zaidi. Wao ni weupe au njano, wenye muundo wa tuta mgongoni, na kichwa cheusi na miguu sita midogo. Wanapofikia kukomaa baada ya wiki 2-3 za kula, hujiigeuza pupa na kuwa mbawakavu kamili katika siku 20-25, huanza mzunguko tena.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia aina sugu.
  • Angalia udhibiti wa karantini katika eneo au katika ngazi ya kitaifa.
  • Fuatilia mashamba mara kwa mara mwanzoni mwa majira ya kuchipua, wakati halijoto inapoongezeka.

Pakua Plantix