Mbiringanya

Mviringisha Jani la Bilinganya

Eublemma olivacea

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Lava hula majani mapya na laini, yakitoa mwonekano wa kuchanika.
  • Majani machanga husokotwa/kuviringishwa kwa urefu.
  • Majani yaliyo sokotwa huwa na rangi ya kahawia na hatimaye hukauka.
  • Katika mashambulizi makubwa, sehemu nzima za mimea huonekana za kahawia na majani hudondoka.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Mbiringanya

Dalili

Ni lava pekee ndio husababisha uharibifu kwenye majani. Dalili za awali huonekana kama majani yaliyo virigwa/sokotwa kwa urefu ambapo ndani yake lava huwepo. Kutoka hapo, lava hao hula tishu za kijani za ndani za majani. Uharibifu huonekana zaidi kwenye sehemu za juu za mmea. Majani yaliyo virigwa yanaweza kuanza kuwa ya kahawia, kunyauka na kukauka. Wakati uharibifu ni mkubwa zaidi, hali ya kuwa kahawia huenea kwenye sehemu nzima za mmea na hufuatiwa na kupukutika kwa majani. Hii inaweza kusababisha upungufu mkubwa wa mavuno ikiwa idadi ya wadudu haitadhibitiwa. Hata hivyo, wadudu hawa ni nadra kuwa tishio kubwa kwa ukuaji wa mimea na mavuno.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Udhibiti wa kibaiolojia kwa kutumia aina za nyigu wanyonyaji kama Cotesia spp. unaweza kusaidia kupunguza maambukizi. Pia, wadudu wawindaji kama mantis au aina za wadudu kobe (ladybird) wanaweza kusaidia kudhibiti wadudu. Nematodes kama Steinernema spp. pia wanaweza kusaidia kudhibiti wadudu hawa.

Udhibiti wa Kemikali

Wakati wote zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibaiyolojia, ikiwa yanapatikana. Ikiwa dawa za kuua wadudu zinahitajika, tumia bidhaa za kupulizia zilizopendekezwa ili kupunguza idadi ya viwavi wakunja majani ya bilinganya.

Ni nini kilisababisha?

Wadudu waliokomaa ni nondo wa ukubwa wa kati, rangi ya kahawia nyepesi hadi kijani ya zeituni, wenye baka kubwa jeusi la pande tatu kwenye eneo la nje la mbawa za mbele. Mbawa za nyuma ni angavu nyeupe. Nondo majike hutaga mayai kwa makundi ya takribani 8-22 kwenye upande wa juu wa majani, mara nyingi kwenye majani machanga. Baada ya siku 3-5, lava huanguliwa. Lava ni wa rangi ya zambarau-kahawia na imara wenye uvimbe wenye ombwe ulio na rangi ya manjano au ya malai (krimu) na nywele ndefu nyuma. Kipindi cha ukuaji wa lava ni takriban wiki 4, kisha lava wanakuwa pupa ndani ya jani lililo virigwa/sokotwa. Baada ya kipindi cha ziada cha siku 7-10, kizazi kipya cha nondo wazima huanguliwa. Kunaweza kuwa na vizazi 3-4 kwa mwaka, kutegemea na hali ya hewa.


Hatua za Kuzuia

  • Inapendekezwa kupanda kwa kuchelewa ndani ya msimu.
  • Panda mimea yenye afya ikiwa na mpango mzuri wa urutubishaji.
  • Angalia mimea yako au mashamba kuona dalili zozote za ugonjwa au wadudu.
  • Ondoa kwa mkono majani yaliyoathirika na viwavi.
  • Ondoa au haribu majani yaliyoathirika, viwavi na taka zako kwa kuzichoma moto.
  • Epuka matumizi holela ya dawa za kuua wadudu ambazo huharibu maadui wa asili wa wadudu waharibifu.

Pakua Plantix