Cosmopolites sordidus
Mdudu
Majani ya kijani hafifu, yanayonyauka na laini yanaweza kuwa dalili za kwanza za migomba iliyoshambuliwa. Mashimo yanayotokana na ulaji au kinyesi kinaweza kuonekana kwanza kwenye vifuko vya majani ya zamani au kwenye sehemu za chini za shina. Lava huchimba vinjia vya chini kwa chini kwenye mashina na mizizi, wakati mwingine kupitia urefu wote wa mashina au mizizi. Katika tishu zilizoathiriwa sana, kuoza hutokea kupitia uozaji wa kuvu, inayoonekana kama rangi nyeusi. Uharibifu kutokana na ulaji na makazi ya vimelea nyemelezi huingilia usafirishaji wa maji na virutubisho, na hivyo kusababisha majani kukauka na kufa kabla ya wakati. Mimea michanga hushindwa kukua na mimea iliyokomaa huonyesha ukuaji uliodumaa. Katika hali mbaya, mimea iliyoathiriwa inaweza kupeperushwa wakati wa hali ya hewa mbaya. Ukubwa na idadi ya mikungu pia hupungua sana.
Hapo awali, idadi kubwa ya wadudu wanaowinda na kula wadudu wengine wamekuwa wakitumika kwa ufanisi ili kudhibiti wadudu hao, miongoni mwao ni baadhi ya spishi za mchwa na mbawakavu. Wawindaji waliofanikiwa zaidi ni mbawakavu wanaojulikana kama Plaesius javanus na Dactylosternus hydrophiloides. Matibabu ya machipukizi kwa maji ya moto (kwa 43°C kwa h 3 au 54°C kwa dakika 20) kabla ya kupanda pia yanafaa. Machipukizi hatimae yapandwe kwenye shamba jipya haraka iwezekanavyo. Kutumbukiza machipukizi kwenye 20% ya mmumunyo/mchanganyiko wa mbegu za mwarobaini (Azadirachta indica) wakati wa kupanda pia hulinda mimea michanga dhidi ya ugonjwa huo.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa inapatikana. Udhibiti unaofaa wa vipekecha mizizi unaweza kufikiwa kwa uwekaji wa viua wadudu kwenye kitako cha mmea. Viua wadudu vya kundi la organofosfati (chloryphos, malathion) vinapatikana pia lakini hizi ni ghali na zinaweza kuwa sumu kwa kidhibiti na mazingira.
Uharibifu wa mazao husababishwa na wadudu waitwao Cosmopolites sordidus na lava wake. Wadudu waliokomaa wanakuwa na rangi ya kahawia iliyokolea hadi kijivu nyeusi, wakiwa na deraya zinazong'aa. Mara nyingi hupatikana kwenye kitako cha mmea, kinachohusishwa na mabaki ya mazao, au kwenye kifuko cha majani. Wadudu hawa hushughulika usiku na wanaishi bila kula kwa miezi kadhaa. Majike hutaga mayai meupe, ya mviringo kwenye mashimo kwenye mabaki ya mazao kwenye udongo au yaliyofichwa kwenye maganda ya majani. Ukuaji wa yai haufanyiki chini ya 12°C. Baada ya kuanguliwa, lava wachanga hutoboa vihandaki kwenye mizizi au kwenye tishu za shina, na kudhoofisha mimea na wakati mwingine kusababisha kuanguka. Wadudu nyemelezi hutumia majeraha yanayosababishwa na kipekecha mizizi kuambukiza mmea. Kuenea kwa wadudu kutoka shamba moja hadi jingine hutokea hasa kupitia nyenzo za upanzi zilizoshambuliwa.