Ndizi

Mnyauko wa Shina

Odoiporus longicollis

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Vishimo vidogo kwenye ala/kifuko-jani cha shina.
  • Utokaji wa utomvu.
  • Umanjano kwenye majani.
  • Ukuaji uliodumaa.
  • Fukusi (kwa jina lingine vidungadunga au vikongomwa) wakubwa wenye rangi nyeusi, kichwa kilichochongoka na deraya inayong'aa.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Ndizi

Dalili

Dalili za kwanza za shambulio la ugonjwa huu ni vishimo vidogo sana na utokwaji wa utomvu wa jeli kwenye kitako cha kifuko cha jani au kwenye shina bandia la mimea michanga. Lava wa kahawia pia huonekana karibu na mashimo. Lava hutengeneza vihandaki kuzunguka shina, na hivyo kusababisha uharibifu mkubwa na kupunguza usafirishaji wa maji na virutubisho hadi kwenye tishu. Majani yanageuka manjano na ukuaji wa mmea unaweza kudumaa. Katika maambukizi makubwa, kudhoofika kwa shina husababisha mimea kuvunjika na kuanguka wakati wa hali ya hewa ya upepo au dhoruba. Tishu hizo hubadilika rangi haraka na kutoa harufu mbaya kwa sababu ya uwepo wa vimelea vya magonjwa nyemelezi kwenye majeraha. Katika mimea iliyoshambuliwa hatua zote za maisha ya fukusi huwepo kwa mwaka mzima. Mikungu au matunda yanaweza yasikue vizuri.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Hapo awali, minyoo-kuru (au nematodi) wa spishi ya Steinernema carpocapsae au aina fulani ya spishi za Arthropodi zimetumiwa kudhibiti fukusi kwa mafanikio fulani. Mbinu nyingine ni kuwaambukiza mbawakavu na vimelea vya magonjwa, kwa mfano na vimelea vya fangasi vya Metarhizium anisopliae.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Dawa za kuua wadudu zenye misombo (mchanganyiko) wa organofosforasi zinaweza kudungwa kwenye shina ili kuua mabuu. Baada ya kuvuna, toa mashina yaliyoathirika na yatie dawa ya kuua wadudu (2 g/l) ili kuua wadudu wanaotaga mayai waliobaki hapo.

Ni nini kilisababisha?

Fukusi wakubwa wana rangi nyeusi, urefu wa karibu 30 mm, na kichwa kilichochongoka na deraya inayong'aa. Mara nyingi hushughulika usiku lakini pia wanaweza kupatikana wakati wa mchana wakati wa miezi ya baridi au siku za mawingu. Wanavutiwa na vitu tete vinavyotolewa na mimea ya ndizi. Majike huchana mpasuo kwenye vifuko vya majani na kutaga mayai yenye rangi ya malai (yaani krimu) juu juu kwa ndani. Baada ya siku 5-8, lava wasio na miguu, wenye rangi mithili ya njano nyeupe huangua na kuanza kula kwenye tishu laini za vifuko vya majani. Lava hawa huchimba njia za chini kwa chini zinazoweza kuwa na urefu wa sentimita 8 hadi 10, kufikia shina, mizizi au mkungu. Wadudu waliokomaa ni warukaji imara na husogea kwa urahisi kutoka mmea mmoja hadi mwingine, wakieneza wadudu kwa njia hii.


Hatua za Kuzuia

  • Hakikisha unatumia nyenzo safi za kupandia kutoka kwenye vyanzo vilivyoidhinishwa.
  • Panda aina za migomba iliyo sugu dhidi ya magonjwa, ikiwa inapatikana.
  • Ondoa na choma moto mabaki yote ya mimea pamoja na mimea iliyovunjika na kuoza ambayo kama si hivyo, inaweza kutumika kama mazalia kwa fukusi wakubwa.
  • Tumia mashina yaliyopasuka kwa wima(longitudo) kwa kuya weka chini kama mitego bandia.
  • Vipande hivi vilivyokatwa huwavutia fukusi majike kula na kutaga mayai yao.
  • Mara tu lava wanapoibuka, vipande hivi hukauka na hatimaye lava hufa kwa sababu ya upungufu wa maji mwilini.

Pakua Plantix