Pieris brassicae
Mdudu
Uharibifu kwenye majani ya nje ni ishara dhahiri ya uwepo wao. Mbali na matundu kwenye majani ya nje, uharibifu kwa kichwa cha kabichi unaweza kuonekana kwenye majani ya ndani unapokata kabichi katikati. Viwavi na vinyesi vyao mara nyingi pia hupatikana kwenye mimea. Mazao yote ya familia ya Brassica yanaathirika, ikiwa ni pamoja na kabichi, koliflawa, kabichi vifundo (Brussels sprouts), swede na tanipu. Aidha, baadhi ya magugu yanaweza kuathiriwa.
Mdudu anaweza kudhibitiwa na vimelea, Cotesia glomerata hushambulia lava/mabuu ya P. brassicae, wakati pteromalus puparam humdhibiti wakati wa hatua ya pupa. Bidhaa zinazotokana na bakteria wanaotokea kiasili, Bacillus thuringiensis au Saccharopolyspora spinosa (spinosad), zina ufanisi mzuri sana zikinyunyiziwa vizuri kwenye sehemu za juu na chini za jani. Dawa hizi za kuua wadudu hazidumu katika mazingira. Minyoo ya vimelea, Steinernema carpocapsae, pia ina ufanisi dhidi ya viwavi na lazima itumike wakati majani yana unyevu, kwa mfano wakati wa hali ya hewa ya baridi.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia na matibabu ya kibayolojia, ikiwa yanapatikana. Bidhaa zinazotokana na viambato amilifu vya pareto, lambda-cyhalothrin au deltamethrin zinaweza kutumika dhidi ya viwavi. Viziduo vya pareto vinaweza kutumika mara kadhaa na hadi siku moja kabla ya kuvuna. Kwa lambda-cyhalothrin na deltamethrin, inashauriwa kutumika si zaidi ya mara 2 na kuheshimu kipindi cha siku saba kabla ya mavuno.
Kipepeo ana mwili mweusi na mabawa meupe yanayong'aa yenye ncha nyeusi inayoonekana kwa wazi kwenye bawa la mbele (na vinukta/vidoa viwili vyeusi kwa majike). Wiki chache baada ya kutokea kwenye hatua ya pupa, majike hutaga mayai ya kijani manjano upande wa chini wa majani. Baada ya kuangua, viwavi huanza kula kwenye tishu za mmea. Viwavi hupekecha ndani ya moyo wa kabichi.