Chrysomelidae
Mdudu
Mbawakavu wakubwa hula kwenye majani. Uharibifu huonekana kama matundu madogo mithili ya risasi (1-2 mm), na mianya midogo ya kutafuna ambayo haikatizi jani. Ubadilikaji mdogo wa majani na kuwa ya manjano unaweza kutokea kuzunguka tishu zilizoharibika. Mizizi hutobolewa na kuwa na vinjia/vihandaki vyembamba, vilivyonyooka huku vikiwa na kina kinachotofautiana kutegemea na aina ya wadudu. Vinundu vidogo vilivyoinuka vinaweza pia kuonekana kwenye sura ya mizizi kama sehemu ya uharibifu.
Vimelea vya kuvu, sabuni za kuua wadudu, au dawa ya Spinosad ya kuua bakteria zinaweza kutumika kupunguza idadi yao. Lava mbawafungo/lacewing (Chrysopa spp.), wadudu aina ya damsel (Nabis spp.) na baadhi ya nyigu vidusia hula au kuua mbawakavu. Baadhi ya minyoo pia huua lava wanaoishi kwenye udongo.
Wakati wote zingatia mbinu jumuishi zikiwa na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibaiyolojia ikiwa yanapatikana. Dawa za kuua wadudu zinapaswa kutumiwa wakati wa kipindi ambacho mbawakavu wanaathirika kirahisi, yaani wanapotokea kwenye majani. Bidhaa zinazotokana na chlorpyrifos hufanya kazi vizuri kudhibiti idadi yao.
Kuna spishi nyingi za mbawakavu viroboto wanaoathiri aina mbalimbali za mimea. Waliokomaa wengi ni wadogo (takriban mm 4), wenye rangi ya weusi, wakati mwingine wakiwa na muonekano wa kung'aa au wa metali. Wana mwili wa umbo la yai na miguu mikubwa ya nyuma kwa ajili ya kuruka. Lava huishi kwenye udongo na kula mizizi, wadudu wakubwa hula mimea michanga. Mbawakavu kiroboto wengi hujificha chini ya mabaki ya mimea wakati wa baridi, kwenye udongo au kwenye magugu kuzunguka mashamba. Huwa wanakuwa hai tena wakati wa majira ya kuchipua. Kutegemea na spishi na hali ya hewa, vizazi 1-4 hukua kwa mwaka.Mbawakavu kiroboto hupendelea hali ya joto na ukavu.