Pseudococcidae
Mdudu
Mkusanyiko wa wadudu walio mithili ya pamba nyeupe huonekana upande wa chini wa majani, mashina, maua, na matunda. Mashambulizi yanaweza kusababisha majani machanga kuwa ya manjano na kujikunja, ukuaji wa mimea kudumaa, na matunda kudondoka mapema. Wadudu hawa hutoa ute/umande wa asali wakati wa wanapofyonza utomvu wa mmea, na hali hii husababisha tishu kunata na hatimae kuvutia bakteria na kuvu wanaoweza kushambulia mmea. Matunda yako hatarini kushambuliwa na yanaweza kuharibika umbo au kufunikwa kabisa na nta. Maji moto wanaweza kuvutiwa na ute wa asali na wanaweza kueneza wadudu waharibifu hadi kwenye mimea mingine. Majani ya zamani yana uwezekano mdogo wa kubadilika umbo au kuharibika.
Inapotokea ishara ya kwanza ya uvamizi mdogo, tumia pamba iliyolowekwa kwenye mafuta au pombe kali kupaka kwenye makundi ya vidung'ata. Unaweza kupulizia mimea kwa sabuni ya kuua wadudu. Mimea iliyo karibu inapaswa kupuliziwa mafuta ya mwarobaini au pyrethrini ili kuzuia kuenea kwa wadudu hawa. Wadudu wa asili wanaosaidia kudhibiti vidung'ata ni pamoja na mbawakimia wa kijani, Nyigu vidusia, nzi weleaji, wadudu kibibi, mdudu kibibi wa kidung'ata (mwangamiza vidung'ata), na kipepeo mla vidung'ata.
Daima zingatia mbinu jumuishi kwa kuchukua hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibaiolojia ikiwa yanapatikana. Matibabu dhidi ya vidung'ata ni magumu kwa sababu wadudu hawa hulindwa na matabaka yao ya nta na nyuzi nyuzi dhidi ya hali mbaya ya mazingira yanayowazunguka. Hata hivyo, kupulizia majani kwa mchanganyilp unaotokana na imidacloprid, acetamiprid, na chlorpyrifos kunaweza kuwa na ufanisi dhidi ya vidukari.
Vidung'ata au Vidukari-sufu ni wadudu wenye umbo la mviringo, wasio na mbawa ambao hupatikana katika maeneo yenye hali ya joto au joto la kiasi. Miili yao inalindwa na tabaka la nta nyembamba inayowafanya waonekane kama pamba. Vidung'ata huchomeka kwenye tishu za mmea sehemu ya mdomo wao mrefu unaochoma mithili ya miba na kufyonza utomvu kutoka kwenye mmea. Dalili zinatokana na kemikali zenye sumu wanazodunga ndani ya mmea wakati wa kula. Mayai ya vidung'ata pia hutagwa kwenye udongo. Baada ya kuanguliwa, tunutu (vidung'ata wachanga) na vidung'ata kamili (wakubwa) wanaweza kutambaa hadi kwenye mimea jirani. Pia wanaweza kusambazwa katika umbali mrefu kwa njia ya upepo, maji moto, wanyama, ndege au wakati wa shughuli za shambani kama vile kupogoa au kuvuna. Wanayo mimea mingine mbadala wanamoweza kuishi kama vile biringanya na viazi vitamu, pamoja na magugu ya aina nyingi. Hali ya joto la uvuguvugu na hewa kavu husaidia mzunguko wa maisha yao na kuongeza ukali wa dalili.