Tikiti

Mbawakawa Hadda

Epilachna vigintioctopunctata

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Uharibifu unaotokana na ulaji wa jani huonekana kati ya mishipa ya majani.
  • Majani hubaki na vishipa.
  • Mashimo ya kina kifupi kwenye matunda.
  • Ukuaji uliodumaa.
  • Upukutikaji mkubwa wa majani.
  • Mbawakawa kamili (wakubwa) wana umbo la mviringo, rangi ya machungwa iliyofifia, na madoa meusi 28 pamoja na manyoya mafupi na laini mgongoni.

Inaweza pia kupatikana kwenye

8 Mazao

Tikiti

Dalili

Mbawakawa wakubwa na lava wote hula majani na wanaweza kusababisha uharibifu mkubwa. Dalili za awali huonekana kama uharibifu unaotokana na kuliwa tishu za kijani kati ya mishipa ya majani. Baadaye, muundo wa tabia za uharibifu unaoitwa skeletonization hutokea, ambapo sehemu ngumu za jani (mshipa mkuu/vena kuu na kikonyo) pekee ndizo zinabaki. Vilevile kunaweza kuwa na mashimo yenye kina kifupi kwenye ngozi ya matunda. Wadudu hawa huharibu miche na kudumaza ukuaji zaidi wa mimea iliyokomaa. Mdudu anaweza kusababisha upukutikaji mkubwa wa majani na upotevu mkubwa wa mavuno, na kwa hivyo ni moja ya wadudu hatari zaidi kwa mimea ya biringanya.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Nyigu vidusia wa familia ya Pediobius wanaweza kutumika kudhibiti wadudu hawa. Nyigu hawa hawa pia hushambulia wadudu-kibibi wenye manufaa, hivyo ni muhimu kutambua wadudu wanaolengwa kwa umakini kabla ya kutumia nyigu vidusia . Vadudu wenye vimelea vya magonjwa wanaweza pia kusaidia kudhibiti idadi ya mbawakawa wanaokula majani. Dawa za kuua wadudu za kibaiolojia zenye bakteria waitwao Bacillus thuringiensis au kuvu Aspergillus spp. zinaweza kutumika kwa kunyunyuzia kwenye majani. Mafuta ya majani ya mbarika/nyoyo, Calotropis procera, na Datura innoxia yanaweza pia kunyunyiziwa kwenye majani. Kutumia majivu kunaweza kupunguza maambukizi katika hatua za awali.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi zikiwa na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibaolojia yanayopatikana. Dawa za kuua wadudu zenye viambato kama fenvalerate na chlorpyrifos zinaweza kutumika kwenye majani, ikiwa inahitajika.

Ni nini kilisababisha?

Mbawakawa wakubwa wana umbo la yai, rangi ya machungwa iliyofifia, na madoa meusi 28 pamoja na manyoya mafupi na laini mgongoni. Mbawakawa jike hutaga mayai yaliyo na umbo la mviringo yenye rangi ya njano (yakiwa na urefu wa milimita 0.4-1 kwa wima) na hutaga katika vikundi vidogo, kwa kawaida kwenye upande wa chini wa majani. Baada ya takribani siku 4, lava wenye rangi ya njano-nyeupe iliyofifia, wakiwa na uti wa mgongo mrefu uliogawanyika na ncha yenye rangi ya nyeusi mgongoni. Lava hukua hadi kufikia urefu wa takriban milimita 6 ndani ya siku kama 18, kutegemea na hali ya joto. Kisha hujongea upande wa chini wa majani na kuingia kwenye hatua ya pupa (mabuu wakubwa). Baada ya siku nyingine 4, kizazi kipya cha mbawakawa wakubwa/kamili huibuka kutoka kwenye vifuko. Wakati wa kipindi cha uzazi (Machi-Okotoba), hali ya ubaridi huwezesha mzunguko wa maisha na ukuaji wa idadi yao. Mbawakawa wanaweza kuishi msimu wote wa baridi kwenye udongo na kwenye rundo la majani makavu.


Hatua za Kuzuia

  • Panda aina za mimea zinazostahimili magonjwa zinazopatikana katika eneo lako.
  • Epuka kupanda mimea ya biringanya ndani ya mashamba yaliyoathirika au karibu na hayo mashamba.
  • Ondoa au epuka kupanda mimea mingine inayoweza kuhifadhi wadudu karibu na shamba lako.
  • Mwagilia maji vizuri ili kuifanya mimea yako iendelee kuwa katika hali nzuri.
  • Kagua mimea yako au shamba lako ili kugundua uwepo wa dalili zozote za wadudu.
  • Chagua kwa uangalifu na haribu lava pamoja mbawakawa wakubwa waliopo kwenye vitalu au mashamba.
  • Ondoa au haribu mimea iliyoathirika na mabaki ya mimea kwa kuyachoma moto.

Pakua Plantix