Mbiringanya

Nzi Weupe

Aleyrodidae

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Madoa ya manjano kwenye majani.
  • Ukungu mithili ya unga mweusi hujitokeza.
  • Ubadilikaji umbo wa jani na kujikunja au kuwa na umbo la kikombe.
  • Ukuaji uliodumaa.
  • Wadudu wadogo weupe au njano.

Inaweza pia kupatikana kwenye

45 Mazao

Mbiringanya

Dalili

Inzi weupe waliokomaa na tunutu(nzi wachanga) hufyonza utomvu wa mimea na kutoa maji maji ya asali kwenye majani, mashina na matunda. Madoa ya klorotiki (yanayotokana na majani kubadilika rangi na kuwa ya njano) na kuvu/ukungu mithili ya majivu hujitokeza kwenye tishu zilizoathirika. Wakati wa maambukizi makubwa, madoa haya yanaweza kuungana na kusambaa kote kwenye jani zima, isipokuwa sehemu inayozunguka vishipa jani. Baadaye majani yanaweza kubadilika umbo, kujikunja au kuwa na umbo la kikombe.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Suluhu za kibayolojia zitatofautiana kutegemeana na aina mahususi za inzi weupe wanaohusika pamoja na mazao. Dawa za asili zinazotokana na mafuta ya tufaha ya sukari (Annona squamosa), pyrethrins, sabuni za kuua wadudu, mbegu za mwarobaini (NSKE 5%), mafuta ya mwarobaini (5ml/L maji) yanapendekezwa. Kuvu vimelea ni pamoja na Beauveria bassiana, Isaria fumosorosea, Verticillium lecanii, na Paecilomyces fumosoroseus.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Inzi weupe kwa haraka hujenga usugu kwa dawa zote za kuua wadudu, hivyo basi, inapendekezwa kutumia kwa mzunguko bidhaa tofauti tofauti za madawa. Tumia bidhaa za madawa zinazotokana na au michanganyiko ya bifenthrin, buprofezin, fenoxycarb, deltamethrin, azadirachtin, lambda-cyhalothrin, cypermethrin, pyrethroids, pymetrozine au spiromesifen ili kudhibiti wadudu. Fahamu kuwa hatua za kuzuia mara nyingi zinatosha kupunguza idadi ya wadudu na kufikia viwango visivyo na madhara.

Ni nini kilisababisha?

Inzi-weupe ni wadudu wanaopatikana kwa wingi kwenye mazao mbalimbali yanayolimwa katika mashamba wazi na kwenye vitalu nyumba(greenhouses). Wana urefu wa takribani 0.8-1 mm na wana miili na mbawa zote mbili zilizofunikwa na kitu mithili ya unga mweupe hadi manjano, na kutoa nta. Mayai yanatagwa upande wa chini wa majani. tunutu(nzi wachanga) wanakuwa na rangi ya manjano hadi nyeupe, umbo bapa, umbo la yai, na rangi ya kijani iliyofifia. Wadudu wakubwa/waliokoma hawawezi kuishi bila kula mimea kwa zaidi ya siku chache. Mara nyingi hupatikana upande wa chini wa majani, na ikiwa wanasumbuliwa, watajitokeza na kuunda wingu. Wanastawi katika hali ya joto na ya ukavu. Baadhi ya inzi weupe husambaza virusi kama vile virusi wa kukunja jani njano la nyanya, maarufu kama rasta au kama kirusi cha michirizi kahawia wa mihogo.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia mazao ya mseto ambayo huvutia au kuzuia inzi weupe (kama vile, nasturtiums, zinnias, hummingbird bush, pineapple sage, bee balm ).
  • Panda mimea mirefu kama vile mahindi, mtama au uwele katika mistari yenye msongamano na hivyo kuwa kama mazao ya mpaka.
  • Shauriana na majirani zako ili kuhakikisha mnapanda wakati sahihi, sio mapema sana na wala sio kwa kuchelewa sana.
  • Tumia nafasi ndogo kati ya mimea (karibu karibu) wakati wa kupanda.
  • Angalia ishara za uwepo wa inzi weupe kwenye miche mipya au kwenye miche iliyopandikizwa.
  • Kagua shamba lako kwa kutumia mitego ya manjano inayonata (20/ekari).
  • Hakikisha uwekaji wa mbolea wenye uwiano.
  • Usitumie dawa za kuua wadudu zenye wigo mpana ambazo zinaweza kuathiri wadudu wenye manufaa.
  • Ondoa majani yenye mayai au lava juu yake.
  • Dhibiti magugu na mimea mbadala inayohifadhi wadudu wa magonjwa kwenye shamba na kuzunguka shamba.
  • Ondoa mabaki ya mimea kutoka kwenye shamba au kitalu nyumba (greenhouse) baada ya mavuno.
  • Panga muda mfupi wa kuacha shamba bila kupanda wakati wa majira ya joto.
  • Nailoni za kitalu nyumba zinazofyonza Urujuani (ultraviolet) zinaweza kupunguza mashambulizi.
  • Tumia kilimo mseto na mimea ambayo haina uwezekano wa kuathiriwa.

Pakua Plantix