Nyingine

Mbawakawa wa Gome la Mti wa Matunda

Scolytus mali

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Vishimo na kinyesi cha wadudu kwenye shina au matawi ya miti yenye mfadhaiko.
  • Endapo gome limekatwa na kuondolewa, mpangilio wa vihandaki unaweza kupatikana moja kwa moja kwenye safu laini za nje ya mti.
  • Tabia hii ya vihandaki inafanana na Mayan quipu.

Inaweza pia kupatikana kwenye

5 Mazao
Tufaha
Aprikoti
Cheri
Mpichi
Zaidi

Nyingine

Dalili

Kwa kawaida majike huchagua miti iliyofadhaika au miti michanga ili kutaga mayai yao. Kwa sababu magome yake ni imara zaidi, miti yenye afya huwa na uwezekano mdogo wa kushambuliwa. Mashimo ya kutokea au kuingilia yakiwa na vinyesi vya wadudu yanaweza kupatikana kwenye shina au matawi. Ikiwa gome limekatwa na kuondolewa, mpangilio wa vihandaki unaweza kupatikana moja kwa moja kwenye kwenye safu laini za nje ya mti. Majike hutafuna na kutengeneza vinjia au vihandaki vya mama ambavyo ni vyembaba vya wima vya urefu wa takribani sentimeta 5-6 (hadi sentimeta 10 cm), na upana wa milimeta 2. Majike hawa wanapofanya hivyo, hutaga mayai kwenye vishimo vidogo kwenye pande za vihandaki. Baada ya kuanguliwa, lava/funza huchimba vinjia au vihandaki vifupi na vyembamba chini ya gome, kuanzia kwenye handaki la mama na karibu kabisa. Tabia hii ya kuchimba vihandaki inafanana Mayan quipu.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Scolytus mali ina idadi kubwa ya wanyama wanaowinda wanyama wengine lakini tafiti chache zimeangalia uwezekano wa matumizi yao kama udhibiti wa kibiolojia shambani. Aina nyingi za ndege huwinda mabuu ya Scolytus mali. Nyigu wa vimelea vya Braconid wa spishi Spathius brevicaudis pia wanaweza kuwa na ufanisi katika kudhibiti idadi ya mbawakawa. Nyigu wengine wa aina ya Chalcid pia wanaweza kutumika (Cheiropachys colon au Dinotiscus aponius, miongoni mwa wengine).

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Matibabu ya viuatilifu ni muhimu ikiwa idadi ya mbawakawa itafikia viwango vya kushambuliwa na inakuwa na ufanisi zaidi wakati wa mbawakawa wakubwa kuruka. Hakuna dawa za kuua wadudu zinazopatikana kwa sasa za kukabiliana na Mbawakawa wa Gome la Mti wa Matunda.

Ni nini kilisababisha?

Dalili zinazoonekana kwenye miti ya matunda husababishwa na mbawakawa anayefahamika kama Scolytus mali. Mabuu ya wadudu hawa ni xylophagous, kumaanisha kwamba wanakula kutoka kwenye safu laini za nje ya mti iliyo chini ya gome. Mbawakawa wakubwa wana mng'ao wa kahawai-nyekundu, na kichwa cheusi na urefu wa takribani milimeta 2.5 hadi 4.5. Majike kwa kawaida huchagua miti iliyodhoofika, kisha huchimba shimo kupitia gome na kutoboa handaki kwenye safu laini za nje ya mti. Mayai huwekwa kando ya kihandiki hiki cha mama, ambacho kinaweza kufikia urefu wa hadi sentimeta 10. Baada ya kuanguliwa, lava/funza hutoboa vihandaki vifupi na vyembamba chini ya gome, kuanzia kwenye handaki la mama na karibu vikiwa wima na handaki la mama. Wakati wa majira ya kuchipua, mabuu hupanda kwenye kiota. Katika halijoto ya kawaida ya joto (18-20°C), mbawakawa waliokomaa huangua mayai, huchimba handaki kupitia gome na kisha kuruka hadi kwenye miti mingine inayofaa kuanza mzunguko mpya. Mashambilizi ni ishara ya kudhoofika kwa miti ambako kupo, na husababishwa kwa mfano na maambukizi ya vimelea vya ukungu/kuvu au hali mbaya ya udongo.


Hatua za Kuzuia

  • Hakikisha lishe bora kwa miti.
  • Hakikisha unamwagilia maji ya kutosha lakini usizidishe maji.
  • Usihifadhi kuni karibu na miti ya matunda.
  • Tumia mitego ya homoni harufu kudhibiti idadi ya wadudu.
  • Miti ya mitego au matawi ya mitego yanaweza pia kuwa na ufanisi.
  • Kata na kuchoma matawi au miti iliyoambukizwa.

Pakua Plantix