Tufaha

Kidukari sufu

Eriosoma lanigerum

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Kunyauka na umanjano wa majani na mashina.
  • Vikwachu (vidonda vya mti) na uvimbe kwenye gome, mashina na mizizi.
  • Kutanda kwa vitu mithili ya sufu nyeupe kwenye maeneo ya kulisha.
  • Ni rahisi kuathiriwa na fangasi (kuvu) nyemelezi.
  • Ukuaji uliodumaa.

Inaweza pia kupatikana kwenye

3 Mazao

Tufaha

Dalili

Wadudu wenye nywele nyeupe wanaweza kuonekana wakila kwenye vichipuzi, vitawi vichanga, matawi, mashina na hata kwenye mizizi. Majani yaliyojipinda, majani ya manjano, ukuaji duni, na ufaji poleple wa matawi ni matokeo ya shughuli hii. Kutanda kwa vitu mithili ya sufu nyeupe na umande wa asali huonekana karibu na maeneo ya kulisha. Juu ya gome na shina, maendeleo ya vikwachu (vidonda) na uvimbe pia ni tabia ya ugonjwa huu. Aina za vidukari sufu vilivyo chini ya ardhi pia hushambulia mizizi na kusababisha uundaji wa upanukaji wa kuvimba au mafundo makubwa. Kasoro za usafiri wa maji na virutubisho unamaanisha kuonekana kwa rangi ya manjano kwenye miti. Vinundu hivi vya mti huongezeka ukubwa mwaka hadi mwaka kutokana na kulisha vidukari. Vidonda vinavyosababishwa na wadudu hao na uwepo wa umande wa asali pia huvutia kuvu nyemelezi ambao wanaweza kufunika tishu zilizoambukizwa na ukungu wa masizi. Mimea michanga hung’olewa kwa urahisi inaposhambuliwa.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Michanganyiko ya dawa ya kunyunyizia ni lazima iweze kupenya utando wa sufi inayotolewa na vidukari ili kuwaua. Mchanganyiko uliozimuliwa wa pombe au dawa za sabuni za kuua wadudu zinaweza kumwagiwa juu ya madoa ya sufi ili kuwasumbua. Mafuta ya kiikolojia au ya mwarobaini (2-3 ml/l maji) yanaweza pia kunyunyiziwa juu ya miti. Ufunikaji mzuri na ufuatiliaji wa dawa siku 7 baada ya kutumia kwa mara ya kwanza ni muhimu. Vimelea au wadudu walao wadudu wengine kama vile mbawakimia, wadudu-vibibi(Exochomus quadripustulatus), mabuu ya nzi mweleaji, na nyigu wa vimelea (Aphelinus mali) wanaweza kusaidia kudhibiti idadi ya wadudu. Makazi bandia hukuza idadi ya wadudu wanaokula wadudu wengine, kwa mfano wadudu-koleo.

Udhibiti wa Kemikali

Wakati wote zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Udhibiti kwa njia ya kemikali (madawa) unaweza kutumika ama kwa ajili ya kukinga au baada ya ugunduzi wa magonjwa. Matibabu ya hatua kwa hatua yanaweza kuwa msaada katika kuzuia vidukari kula kwenye mimea iliyotibiwa. Kwa bahati mbaya, wanaweza pia kuwa na madhara kwa wadudu wenye manufaa. Dawa tendaji hujumuisha michanganyiko inayotokana na deltamethrin, lambda-cyhalothrin, na acetamiprid. Carbamates na pyrethroids zinapaswa kuepukwa kwani huchochea milipuko ya vidukari kwa kuua vimelea na wadudu wengine wanaokula vidukari. Miti iliyo na maua haipaswi kunyunyiziwa dawa kwa sababu itahatarisha wadudu wanaochavusha.

Ni nini kilisababisha?

Dalili husababishwa na shughuli ya kulisha vidukari sufu (Eriosoma lanigerum). Tofauti na vidukari wengi, vidukari sufu hunyonya maji kutoka kwenye mashina ya mti na vichipuzi, badala ya kutoka kwenye majani. Mdudu huyu ana sifa ya ufunikaji kwa wa nta yake nzito na nyeupe mithili ya sufu. Aidha, vidukari sufu huishi kipindi chote cha majira ya baridi kwenye nyufa au vidonda vya magome kuzunguka maeneo ya zamani ya malisho (kama vile majani, matawi, vichipuzi, n.k) ya mimea inayobeba wadudu hawa. Kadiri hali ya joto inavyoongezeka katika majira ya kuchipua, vidukari huwa hai tena na kupanda juu ya vichipuzi, na matawi katika kutafuta maeneo muafaka kwao (maeneo yenye gome nyembamba). Huko, hula kwa pamoja, kunyonya maji maji ya mti kutoka chini ya gome, na kuanza kutoa nywele laini mithili ya sufu ambazo hatimaye zilifunika kundi la wadudu. Vimelea vya magonjwa kisha vinaweza kutawala majeraha haya wazi ya gome. Wakati wa majira ya joto, wadudu wakubwa huota mbawa na kuruka mbali kutafuta mimea mipya. Miti ya elmu iliyo karibu na bustani huongeza uhamiaji wa vidukari kwenye bustani ya tufaha.


Hatua za Kuzuia

  • Chagua aina ya mimea ambayo ni sugu dhidi ya magonjwa ikiwa inapatikana.
  • Katika mashambulizi madogo, wadudu wanaweza kufuatiliwa na kusuguliwa kwa brashi.
  • Tumia virutubisho vya ziada au mbolea ili kuimarisha mimea.
  • Epuka matumizi makubwa ya dawa za kuua wadudu kwani zinaweza kupunguza idadi ya wadudu wenye manufaa.
  • Upogoaji matawi mwishoni mwa majira ya joto ili kuondoa makundi ya wadudu.
  • Ondoa mashina machanga na matawi yaliyoathirika.
  • Ondoa vichipuzi sehemu ya chini ya mmea ili kutengeneza mazingira yasiyo rafiki kwa vidukari.
  • Tumia rangi za kibiashara kupaka sehemu kubwa za mmea zilizokatwa ili kuzuia makundi ya vidukari.
  • Usipande miti ya mwelmu(elm) karibu na bustani ya miti ya tufaha.

Pakua Plantix