Thysanoptera
Mdudu
Mabaka madogo ya rangi ya fedha huonekana kwenye upande wa juu wa majani, athari inayojulikana kama 'kuwa rangi ya fedha'. Mabaka hayo hayo yanaweza kuonekana kwenye petali wakati rangi ya asili ikiwa imeondolewa. Upande wa chini wa majani, vithiripi na mabuu yake hukaa pamoja katika vikundi wakiwa pamoja na madoa ya kinyesi chao cheusi. Majani ya mimea iliyoathiriwa ni ya manjano, hunyauka, kuharibika au kusinyaa. Kulisha wakati wa chipukizi au ukuaji wa maua baadaye husababisha maua au matunda yenye makovu, kudumaa au kuharibika umbo mtawalia na kupoteza mavuno.
Baadhi ya hatua za udhibiti wa kibayolojia zimeshatengenezwa kwa ajili ya vithiripi maalum. Dawa ya kuua wadudu iitwayo Spinosad kwa ujumla ina ufanisi zaidi dhidi ya vithiripi kuliko dawa nyingine yoyote ya kikemikali au michanganyiko mingine ya kibayolojia. Hudumu kwa wiki 1 au zaidi na husogea umbali mfupi kwenye tishu zilizopuliziwa dawa. Inaweza, hata hivyo, kuwa sumu kwa baadhi ya maadui wa asili (kwa mfano, wadudu wanaokula wadudu wenzao, mabuu ya nzi waeleaji) na nyuki. Kwa hiyo, usitumie dawa ya spinosad kwa mimea inayochanua maua. Kwa suala la kushambuliwa maua, mchanganyiko wa vitunguu (vilivyokamuliwa/ziduliwa) na baadhi ya dawa za kuua wadudu pia inaonekana kufanya kazi vizuri. Kwa zile zinazoshambulia majani lakini sio maua, jaribu mafuta ya mwarobaini au pyrethrins asilia (yaani dawa inayotokana na pareto), hususani kwenye sehemu ya chini ya majani. Matumizi ya matandazo ya UV yenye kuakisi sana (matandazo ya kuakisi yaliyo na metali) yamependekezwa.
Wakati wote zingatia mbinu jumuishi na hatua za kukinga pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Kutokana na viwango vya juu vya uzazi na mzunguko wa maisha yao, vithiripi wamejenga usugu dhidi ya makundi mbalimbali ya dawa za kuua wadudu. Viuwa wadudu vinavyoweza kugusana vyema ni pamoja na fipronil, imidacloprid, au acetamiprid, ambavyo katika bidhaa nyingi huunganishwa na piperonyl butoxide ili kuongeza athari zao.
Mabuu na wadudu waliokua hula kwenye tishu za mimea. Vithiripi wana urefu wa milimeta 1-2, wana rangi ya njano, nyeusi au rangi zote mbili. Aina zingine za Vithiripi wana jozi mbili za mbawa, wakati zingine hazina mabawa kabisa. Wadudu hawa hujificha kwenye mabaki ya mimea au kwenye udongo au kwenye mimea mbadala inayoweza kubeba wadudu hawa. Pia ni wadudu wanaobeba vimelea vya magonjwa mbalimbali yanayosababishwa na virusi. Vithiripi huathiri aina mbalimbali za mimea. Hali ya hewa kavu na ya joto inasaidia sana ukuaji wa idadi ya wadudu, wakati hali ya unyevu inapunguza. Wadudu wakubwa wanaweza kubebwa kwa urahisi na upepo, nguo, vifaa, na vyombo visivyosafishwa vizuri baada ya kazi ya shambani.