Mti wa jamii ya mchungwa

Vidukari

Aphis

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Majani yaliyojipinda na kuharibika umbo.
  • Wadudu wadogo chini ya majani na vijishina (vichipuzi).
  • Ukuaji uliodumaa.

Inaweza pia kupatikana kwenye

59 Mazao
Mlozi
Tufaha
Aprikoti
Ndizi
Zaidi

Mti wa jamii ya mchungwa

Dalili

Idadi ya chini hadi ya wastani kwa kawaida haina madhara kwa mazao. Uwepo wa idadi kubwa ya wadudu-mafuta unaweza kusababisha majani na vichipuzi kujikunja, kunyauka au kuwa vya njano na kusababisha udumavu wa mimea. Kupungua kwa jumla kwa uimara wa mimea kutaonekana. Wadudu-mafuta(viduakari) huzalisha vimajimaji vya asali ambavyo vinaweza kusababisha maambukizi ya ziada yanayotokana na vijidudu nyemelezi, vinavyoonekana kutokana na maendeleo au ukuaji wa kuvu au ukungu kwenye majani. Vimajimaji vya asali pia huvutia mchwa. Hata idadi ndogo ya viduakari (wadudu-mafuta) wanaweza kusambaza virusi kutoka mmea mmoja hadi mwingine kwa njia ya muendelezo.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Kwa suala la maambukizi madogo, tumia mchanganyiko wa sabuni ya kuua wadudu au mchanganyiko unaotokana na mafuta ya mimea, kwa mfano, mafuta ya mwarobaini (3 ml/l). Vidukari pia huathirika kwa urahisi sana na magonjwa ya ukungu wakati wa unyevu. Mnyunyizio wa maji kwenye mimea iliyoathiriwa pia inaweza kuwaondoa.

Udhibiti wa Kemikali

Wakati wote zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Fahamu kwamba, matumizi ya viuatilifu vyenye kemikali vinaweza kusababisha vidukari kuwa sugu kwa zile dawa zinazotumika. Inaweza kupangwa matumizi ya flonicamid na maji kwa uwiano wa (1:20) kwa siku 30, 45, 60 baada ya kupanda (DAS). Fipronil 2 ml au thiamethoxam (0.2 g) au flonicamid (0.3 g) au acetamiprid (0.2 kwa lita moja ya maji) pia inaweza kutumika. Hata hivyo, kemikali hizi zinaweza kuwa na athari mbaya kwa wanyama wanaowinda wanyama wengine, vimelea na wadudu wachavushaji.

Ni nini kilisababisha?

Vidukari au wadudu-mafuta ni wadudu wadogo, wenye mwili laini na miguu mirefu na vipapasio. Ukubwa wao ni kati ya 1/2 milimeta hadi milimeta 2, na rangi ya miili yao inaweza kuwa njano, kahawia, nyekundu au nyeusi, kutegemea na aina ya viduakari. Umbo lao ni kuanzia aina ya wasio na mbawa, ambao kwa ujumla ndio wengi, hadi aina za wenye mbawa, nta au sufu. Hali bora kwa ukuaji wao ni hali ya hewa ya ukavu na joto. Kwa kawaida hutulia na kula kwa makundi kwenye upande wa chini wa majani machanga yaliyolishwa vizuri na kwenye ncha za vichipuzi au vitawi vichanga. Wadudu hawa wanatumia sehemu za midomo yao mirefu kutoboa tishu laini za mmea na kunyonya majimaji. Baada ya uvamizi wa awali mwishoni mwa majira ya kuchipua au mwanzoni mwa kiangazi, idadi ya vidukari hupungua kiasili kutokana na maadui asilia. Aina kadhaa hubeba virusi vya mimea ambavyo vinaweza kusababisha ukuaji wa magonjwa mengine.


Hatua za Kuzuia

  • Dumisha idadi kubwa ya aina tofauti za mimea kwenye shamba.
  • Ondoa mabaki ya mimea yaliyopelekea uzalishaji wa bakteria siku zilizopita.
  • Tumia matandazo yanayoakisi (yanayorudisha) mwanga ili kufukuza idadi ya vidukari wanaovamia mazao.
  • Fuatilia mashamba mara kwa mara ili kutathmini matukio ya ugonjwa au wadudu na kutambua ukali wao.
  • Ondoa sehemu za mmea zilizoambukizwa.
  • Chunguza magugu yaliyopo ndani na kuzunguka shamba.
  • Usimwagilie maji au kuweka mbolea kupita kiasi.
  • Dhibiti idadi ya chungu au mchwa ambao hulinda viduakari (wadudu-mafuta) kwa kutumia utepe unaonata.
  • Punguza matawi ya miti yako au ondoa majani ya chini ya mimea yako ili kuruhusu uingizaji hewa wa sehemu ya juu kabisa ya matawi.
  • Ikiwezekana, tumia vyandarua kulinda mimea.
  • Dhibiti matumizi ya viua wadudu ili usiathiri wadudu wenye faida.

Pakua Plantix