Embe

Utitiri wa Utando wa Jani la Mwembe

Cisaberoptus kenyae

Mchwa

Kwa Ufupi

  • Utando mweupe upande wa juu wa jani.
  • Mabadiliko ya rangi ya jani.
  • Kutokea kwa upukutishaji wa majani.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Embe

Dalili

Utitiri huishi kwa vikundi na hutengeneza utando mweupe au ulio mithili ya nta kwenye upande wa juu wa jani. Utando huu unakua zaidi na kuunda nyuzi nyuzi nyeupe ambazo huimarika na kuwa utando ulio mithili ya rangi ya fedha unaofunika jani lote. Utitiri hawa hufyonza utomvu wa mimea kutoka kwenye majani, na kusababisha ubadilikaji wa rangi. Majani yaliyoathiriwa sana yanaoneka kuwa makavu na yenye rangi ya kahawia-nyeusi(kahawia iliyokolea). Majani yaliyoathirika mara nyingi huanguka baada ya kuwa na rangi ya manjano.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Kwa kuwa ni wadudu wadogo na hawasababishi kupungua kwa mavuno ya matunda, hakuna ulazima wa kuwadhibiti kibaiolojia. Tumia tu mbinu bora za usimamizi wa shamba.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu zinazojumuisha hatua za kukinga pamoja na matibabu ya kibaiolojia, ikiwa yanapatikana. Kwa kuwa ni wadudu wadogo na hawasababishi kupungua kwa mavuno ya matunda, sio lazima kutumia kemikali za kuua utitiri.

Ni nini kilisababisha?

Madhara husababishwa na hatua zote za maisha ya utitiri wa utando wa jani. Utitiri hawa ni wadogo sana, kwa kawaida wana urefu wa takriban milimita 0.2, na hawawezi kuonekana kwa macho. Utitiri hawa wana rangi nyepesi na umbo la biri (cigar), huku mayai yao yakiwa na rangi nyeupe hafifu, ya mviringo, na bapa. Katika hatua zote za maisha, utitiri hawa huishi chini ya utando wa jani na kufyonza utomvu kutoka kwenye mmea. Kwa ujumla, utitiri hawa huambukiza tu miti ya maembe iliyokua kupita kiasi au iliyoachwa bila kutunzwa. Idadi ya utitiri hufikia kilele chake mwezi wa Machi na hupungua mwezi wa Desemba. Mashambulizi huwa makali zaidi wakati wa miezi ya majira ya joto.


Hatua za Kuzuia

  • Pogoa matawi yaliyoathirika baada ya mavuno.
  • Ondoa na haribu majani yenye utando mweupe.
  • Pogoa mimea ili kuongeza kiasi cha mwanga na upitishaji mzuri wa hewa unaofika kwenye majani ili kuzuia na kupunguza mashambulizi ya ugonjwa.

Pakua Plantix