Colomerus vitis
Mchwa
Dalili zinategemeana na aina ya utitiri wanaohusika, aina ya zabibu, na hali za mazingira. Dalili za kawaida zaidi hujitokeza mwishoni mwa majira ya kuchipua, wakati baadhi ya maeneo ya uso wa juu wa majani machanga huvimba kwa juu na kugeuka kuwa uvimbe ulio mithili ya malengelenge. Tabaka la manyoya mafupi na laini, yenye rangi mbalimbali, kuanzia nyeupe hadi nyekundu ya waridi, linaweza kupatikana kwenye vishimo vilivyomo chini ya maeneo haya yaliyoinuka kwa juu. Utitiri wadogo na wenye kupitisha mwanga hulindwa na tabaka hizi nene za manyoya. Baadaye, uvimbe na manyoya yanayowafunika kwa ndani hukauka na kuwa na rangi ya kahawia. Katika baadhi ya nchi, utitiri hawa husababisha aina tofauti ya uharibifu, kwa mfano kupinda kwa kitako cha majani pamoha na kuharibika umbo la vitumba na kujikunja kwa majani.
Utitiri wawindaji wanaofahamika kitaalamu kama Galendromus occidentalis huwinda na kula utitiri wa malengelenge na wameonekana kuwa na ufanisi katika kupunguza idadi yao. Sabuni ya kuua wadudu au mafuta ya mwarobaini yanaweza pia kutumika, tiba hizi zinaweza pia kupunguza idadi ya wadudu wenye manufaa. Zaidi ya hayo, matibabu kwa kutumia salfa inayoyeyuka yanaweza kusaidia.
Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kuzuia na matibabu ya kibaiolojia ikiwa yanapatikana. Dawa ya kuua wadudu aina ya Spirotetramat imetumika kwa mafanikio dhidi ya utitiri wa malengelenge. Hakikisha kuna majani ya kutosha kwa ajili ya kufyonza mchanganyiko wa dawa na tumia dawa hii kila baada ya siku 30. Salfa inayoyeyuka pia inaweza kutumika.
Uvimbe mithili ya malengelenge/upele kwenye majani unasababishwa na utitiri wa Colomerus vitis. Licha ya dalili zilizo dhahiri, utitiri huu hauchukuliwi kuwa ni mdudu hatari kwa zabibu. Wadudu hawa wadogo wanaofyonza utomvu huathiri zaidi mizabibu. Wakati utitiri hawa wanapokula kwenye ngozi ya majani, huingiza dutu zinazofanana na homoni kwenye seli ambazo hubadilisha ukuaji wake, na kusababisha kutokea kwa uvimbe. Utitiri wa malengelenge huishi msimu mzima wa baridi kwenye mmea wa zabibu,kwa mfano wakijificha chini ya magamba ya vitumba. Hatimae wanakuja kuwa katika harakati wakati wa majira ya kuchipua wanapohamia upande wa chini wa majani machanga na kuanza kula kwenye majani hayo. Mwisho mwa majira ya joto, utitiri huyaacha majani na kutafuta maficho dhidi ya baridi. Kufunikwa kwa upande wa chini wa majani kusifananishwe kimakosa na ugonjwa wa kuvu (ukungu) kama vile ubwiri. Dalili zinakuwa kali zaidi wakati wa ukuaji wa haraka wa majani katika hali ya hewa ya unyevu wenye uvuguvugu, lakini utitiri hawa hawaonekani kuwa na athari mbaya kwenye mavuno ya matunda.