Tumbaku

Utitiri wa Maharage

Tetranychidae

Mchwa

Kwa Ufupi

  • Madoa madogo kwenye majani.
  • Utando mdogo kati ya shina na jani.
  • Majani yaliyokauka.
  • Wadudu wadogo, wa kijani hafifu, wenye umbo la mviringo.

Inaweza pia kupatikana kwenye

39 Mazao

Tumbaku

Dalili

Ulaji wa utitiri husababisha kutokea kwa madoa meupe hadi ya manjano kwenye upande wa juu wa majani. Kadiri maambukizi yanavyokuwa makubwa, mwanzoni majani yanaonekana kuwa ya rangi ya shaba nyeusi au ya fedha, kisha yanakuwa yamekakamaa, yanachanika kati ya vishipajani (mishipa ya jani), na hatimaye kuanguka. Mayai ya utitiri yanaweza kupatikana upande wa chini wa majani. Utitiri wenyewe unapatikana hapo, ukijificha kwenye kifukofuko kinachofanana na utando. Mimea iliyoambukizwa itafunikwa na utando unaosokotwa na utitiri. Ncha za mashina zinaweza kuwa na upara na matokeo yake, machipukizi ya pembeni huanza kukua. Katika hali ya uharibifu mkubwa, kiasi pamoja na ubora wa matunda hupungua.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Katika hali ya maambukizi madogo, waoshe utitiri na ondoa majani yaliyoathiriwa. Tumia maandalizi yanayotokana na mafuta ya kanola, basil, soya, na mwarobaini ili kunyunyizia majani kwa umakini na kupunguza idadi ya utitiri. Jaribu pia chai ya vitunguu swaumu, mchanganyiko wa maji na upupu, au mchanganyiko wa sabuni za kuua wadudu ili kudhibiti idadi yao. Shambani, tumia udhibiti wa kibiolojia unaolenga mimea maalum inayohifadhi utitiri kwa kutumia utitiri wawindaji (kwa mfano Phytoseiulus persimilis) au dawa ya kibiolojia Bacillus thuringiensis. Matibabu ya pili ya kunyunyizia yanahitajika siku 2 hadi 3 baada ya matibabu ya awali.

Udhibiti wa Kemikali

Daima fikiria kutumia mbinu jumuishi zikiwemo hatua za kinga pamoja na matibabu ya kibiolojia ikiwa yanapatikana.Utitiri hawa ni vigumu kuwadhibiti kwa kutumia dawa za kuua wadudu za aina ya acaricides kwa sababu idadi kubwa huunda usugu dhidi ya kemikali tofauti baada ya miaka michache ya matumizi. Chagua madawa ya udhibiti wa kikemikali kwa uangalifu ili yasiathiri idadi ya wadudu wanaowinda na kula wadudu waharibifu. Dawa za kuua wadudu zinazotokana na salfa inayoweza kuyeyuka (3 g/l), spiromesifen (1 ml/l) au abamectin zinaweza kutumika kwa mfano (uzimuaji/kuzimua kwenye maji). Matibabu ya upili ya kunyunyiza yanahitajika siku 2 hadi 3 baada ya matibabu ya awali ni muhimu.

Ni nini kilisababisha?

Uharibifu husababishwa na utitiri kutoka kwa jenasi ya Tetranychus, hasa T. urticae na T. cinnabarinus. Jike la utitiri lililopevuka lina urefu wa mm 0.6, lina rangi ya kijani hafifu na madoa mawili meusi kwenye mwili wake wa mviringo, na nywele ndefu mgongoni. Majike yanayoishi majira ya baridi yana rangi nyekundu. Wakati wa majira ya kuchipua, majike hutaga mayai ya duara na yanayopitisha mwanga upande wa chini wa majani. Tunutu ni wa rangi ya kijani hafifu wakiwa na alama nyeusi upande wa juu. Utitiri hujikinga na utando kwenye upande wa chini wa majani. Wadudu hawa hustawi katika hali ya hewa kavu na yenye joto na huzaa vizazi hadi 7 kwa mwaka katika hali hizi. Kuna aina nyingi za mimea mbadala inayotunza wadudu hawa, ikijumuisha magugu.


Hatua za Kuzuia

  • Panda aina za mbegu zinazostahimili magonjwa ikiwa zinapatikana.
  • Fuatilia shamba lako mara kwa mara na kagua upande wa chini wa majani.
  • Vinginevyo, tikisa majani ili kudondosha wadudu wachache juu ya karatasi nyeupe.
  • Ondoa majani au mimea iliyoathiriwa.
  • Ondoa mimea ya upupu na magugu mengine kutoka kwenye mashamba.
  • Nyunyizia maji kwenye njia na maeneo mengine yenye vumbi mara kwa mara ili kuepuka hali ya vumbi shambani.
  • Mwagilia mazao yako mara kwa mara kwa sababu miti na mimea inayokosa maji ina ustahimilivu mdogo dhidi ya uharibifu unaotokana na utitiri.
  • Dhibiti matumizi ya dawa za kuua wadudu ili kuruhusu ustawi wa wadudu wenye manufaa ambao hula wadudu waharibifu kama vile utitiri.

Pakua Plantix