Pectobacterium carotovorum subsp. carotovorum
Bakteria
Mwanzoni, madoa yaliyotota maji yanaundwa. Madoa haya huongezeka ukubwa na kuwa yaliyozama na laini. Tishu za mimea zilizo chini ya madoa zinakuwa zimeoza na kubadilika rangi, kutoka rangi ya krimu hadi nyeusi. Katika hali ya maambukizi makali, majani, mashina, na mizizi vinaweza kuoza kabisa. Harufu kali inaweza kusikika
Mpaka leo hatufahamu uwepo wa njia yoyote ya kibayolojia ya kudhibiti ugonjwa huu. Ikiwa unajua njia yoyote yenye mafanikio ya kupunguza kiwango au ukali wa dalili, tafadhali wasiliana nasi.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Hatua za udhibiti hufanywa kwa njia ya kuzuia kwani bakteria mwenyewe hawezi kuponywa. Ili kuzuia na kukomesha vimelea vya bakteria tumia dawa za kuua kuvu zinazotokana na shaba. Ciprofloxacin pia ni kizuizi kizuri cha ugonjwa huo.
Uharibifu husababishwa na bakteria Pectobacterium carotovorum, ambao huishi kwenye udongo na kwenye mabaki ya mazao. Bakteria hawa huingia kwenye mazao kupitia majeraha yanayosababishwa na zana za kilimo, wadudu, uharibifu wa mvua ya mawe au mianya ya asili. Kimelea huenezwa na wadudu, zana za kilimo, uhamishaji wa miche iliyoathirika, udongo au maji yaliyochafuliwa. Tatizo huwa kubwa wakati wa hali ya hewa ya unyevu na joto la 25-30°C, na huwa mbaya zaidi wakati mimea inapokuwa na upungufu wa kalsiamu. Ugonjwa hutokea shambani na pia mahali pa kuhifadhia.