Xanthomonas axonopodis pv. punicae
Bakteria
Dalili za kwanza huonekana baada ya siku 2-3 za maambukizi. Madoa ya mviringo yaliyotota maji yenye rangi ya njano yanaweza kupatikana kwenye sehemu za mmea. Upukutishaji wa majani mapema hutokea katika hali mbaya. Madoa ya mviringo huonekana kama vidonda visivyo na mpangilio katika hatua za baadaye. Hatua kwa hatua, katikati ya madoa tishu hufa na hugeuka kahawia nyeusi. Vimelea pia husababisha kugugunwa na kupasuka kwa shina na matawi. Katika hatua za juu za maambukizi, kufa kwa tishu hutokea kwenye majani na matawi. Ugonjwa husababisha tunda zima kupasuka, hatimaye kugeuza tunda lote kuwa kavu na jeusi. Mimea huathirika katika hatua zote za ukuaji.
Tumia vidhibiti vya kibaolojia kama vile Bacillus subtilis, Pseudomonas fluorescence na Trichoderma harzianum. Loweka majani ya mwarobaini kwenye mkojo wa ng'ombe na upulizie dawa ili kudhibiti wadudu na vimelea vya magonjwa ya mimea. Tumia 40% ya viziduo ya majani ya Tulsi ikifuatiwa na mafuta ya mbegu za Mwarobaini. Pia, weka viziduo vya vitunguu saumu, shina la Meswak na majani ya Patchouli kwa 30% kwa kila mchanganyiko.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia, ikiwa yanapatikana. Hakuna udhibiti mzuri wa kemikali kwa ugonjwa huu ambao umeshagunduliwa. Chaguzi kadhaa za usimamizi zinazohusisha utumiaji wa antibaiotiki, kemikali na matibabu mengine ya kitamaduni yamezingatiwa, lakini matibabu ya kemikali hayafanyi vizuri. Kemikali kama mchanganyiko wa Bordeaux, Captan, copper hydroxide, bromopol,na antibiotic streptocycline inaweza kutumika peke yake au kwa mchanganyiko.
Uharibifu husababishwa na bakteria anayeenezwa na upepo Xanthomonas axonopodis pv. Punicae. Kimelea hiki huambukiza aina mbalimbali zinazolimwa bila kujali hatua ya ukuaji wa mimea hiyo. Bakteria huingia kupitia uwazi/matundu ya asili na majeraha. Bakteria hupita kwenye majani, shina na matunda ya mimea iliyoambukizwa. Kunyesha kwa mvua, wadudu na zana zilizochafuliwa za kupogoa husaidia kueneza magonjwa ndani ya eneo husika. Joto la juu la siku na unyevu wa chini huchangia ukuaji wa vimelea. Joto bora kwa ukuaji wa bakteria ni 30 ° C. Mvua na matone ya kunyunyizia dawa, maji ya umwagiliaji, zana za kupogolea, wanadamu na wadudu ni wahusika wa kuenea kwa upili kwa bakteria. Ugonjwa huu hupunguza uwezekano wa kuuzika kwa matunda sokoni.