Mbiringanya

Jani Dogo la Biringanya

Phytoplasma

Bakteria

Kwa Ufupi

  • Kupungua kwa ukubwa wa majani.
  • Majani kugeuka rangi na kuwa ya njano.
  • Kuzuia uzalishaji wa matunda.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Mbiringanya

Dalili

Mimea iliyoathirika inajulikana kwa kuwa na majani madogo, laini, membamba, na yaliyoharibika mwonekano huku yakiwa na rangi ya manjano hafifu. Aina ya mimea yenye miiba inakuwa laini na kupoteza miiba yake. Mimea kwa ujumla huwa na ukuaji uliodumaa na pingili fupi pamoja na vikonyo. Hufanya mmea kuwa na idadi kubwa ya matawi na mizizi kuliko mimea yenye afya, na hivyo mmea kuwa na muonekano mithili wa kichaka, na hivyo pia hufahamika kama Witches Broom, au Fagio la Wachawi. Sehemu za maua huharibika na mara nyingi zinakuwa tasa (hazina uwezo wa kuzaa). Matunda yanayokua huwa magumu,imara, na kushindwa kukomaa. Kadiri ugonjwa unavyoendelea, majani mapya yanayokua yanakuwa na ukubwa wa 1/3 - 1/4 ya ukubwa wake wa asili.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Wadudu wenye manufaa kama vile mbawakimia, damsel bug, na minute pirate bug ni wawindaji wakali wa hatua zote za yai na lava za wadudu hawa.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibaiolojia, ikiwa yanapatikana. Imidacloprid, Cypermethrin, na Dimethoate zinaweza kutumika kupunguza wadudu wanaobeba magonjwa.

Ni nini kilisababisha?

Dalili hizi husababishwa na vimelea vinavyofanana na bakteria vinavyoitwa phytoplasma. Uambukizaji kutoka mmea mmoa hadi mwingine hufanyika hasa kupitia wadudu wanaobeba magonjwa, aina mbalimbali za waruka jani, hususani Hishimonas phycitis. Ugonjwa huu unaweza kuathiri mimea katika hatua zote za ukuaji.


Hatua za Kuzuia

  • Panda aina za mimea zinazostahimili magonjwa kama vile Pagoda.
  • Epuka kulima mimea inayohifadhi magonjwa kama vile Pilipili.
  • Toa nafasi ya kutosha kati ya mmea na mmea wakati wa kupanda, kwa usahihi 90x75 cm.
  • Rekebisha wakati wa kupanda ili kuepuka msimu wa kilele cha wadudu wanaosambaza ugonjwa.
  • Chunguza shamba mara kwa mara ili kugundua uwepo wa dalili za mashambulizi ya mruka-jani (mvuka jani) ili kuhakikisha shamba halina ugonjwa.
  • Ondoa na haribu mara moja mimea iliyoathirika.
  • Ondoa mimea (magugu) inayohifadhi wadudu/magonjwa.
  • Panda mimea ya kizuizi kuzunguka shamba lako; mimea ambayo itazuia wadudu wanaobeba magonjwa kushambulia mazao yako moja kwa moja.
  • Hifadhi maadui wa asili na wadudu wenye manufaa.

Pakua Plantix