Xanthomonas axonopodis pv. manihotis
Bakteria
Dalili hujumuisha mabaka, kunyauka, kufa kwa matawi, na kufa kwa tishu za mishipa. Kwenye majani, madoa ya tishu zilizo kufa yenye umbo la pembe huonekana, yaliyopunguzwa na mishipa midogo na kusambazwa isivyo kawaida kwenye lamina. Madoa haya mara nyingi huzungukwa na ukanda angavu ulio badilika rangi. Madoa huanza kama vidonda vyenye unyevunyevu, rangi ya kahawia, ambavyo kwa kawaida vipo sehemu ya chini ya mmea mpaka vinapoanza kupanuka na kuungana, na mara nyingi kusababisha kifo cha jani lote. Mkusanyiko wa utomvu wa gundi hutokea kwenye majeraha na mishipa ya majani. Mchakato huu huanza na kimiminika cha dhahabu laini ambacho baadaye huganda na kuunda mabaki yenye rangi ya kaharabu. Mashina na vikonyo vichanga vinaweza kupasuka baada ya maambukizi, pia vikitoa utomvu wa gundi.
Kuchovya mbegu zilizoambukizwa kwenye maji ya moto kwa nyuzi 60°C kwa dakika 20, kisha kukausha kwa tabaka nyembamba kwenye joto la nyuzi 30°C usiku kucha au nyuzi 50°C kwa saa 4, hupunguza idadi ya bakteria kwa kiasi kikubwa. Mbegu zinaweza pia kuzamishwa kwenye maji na kupashwa moto kwenye oveni ya microwave hadi joto la maji lifikie nyuzi 73°C, kisha maji hayo kutupwa mara moja.
Kila wakati zingatia mbinu jumuishi kwa kuchukua hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibaolojia ikiwa yanapatikana. Hakuna udhibiti wa moja kwa moja wa kemikali dhidi ya ugonjwa wa bakiteria wa mihogo uliopo kwa sasa. Tafadhali tujulishe ikiwa unajua njia yoyote. Pia, toa taarifa kuhusu uwepo wa vimelea hivi kwa mamlaka za karantini.
Dalili husababishwa na aina ya bakteria Xanthomonas axonopodis anaeshambulia mimea ya mihogo (manihotis) kwa urahisi. Ndani ya mazao (au mashamba), bakteria husambazwa na upepo au matone ya mvua. Vifaa vilivyochafuliwa pia ni njia muhimu ya kusambaza, pamoja na shughuli za binadamu na wanyama kwenye mashamba, hasa wakati au baada ya mvua. Hata hivyo, tatizo kubwa la vimelea hivi ni usambaaji wake kwa umbali mrefu kupitia mbegu za kupanda ambazo hazionyeshi dalili dhahiri, vipandikizi na mbegu, hasa barani Afrika na Asia. Mchakato wa maambukizi na maendeleo ya ugonjwa unahitaji unyevunyevu wa asilimia 90-100 kwa saa 12, na joto bora kati ya nyuzi 22-30°C. Bakteria hukaa hai kwa miezi kadhaa kwenye mashina na gundi, wakianza tena shughuli zao wakati wa vipindi vya mvua. Mwenyeji mwingine pekee wa bakteria huyu anayejulikana ni mmea wa mapambo Euphorbia pulcherrima (poinsettia).