Dickeya zeae
Bakteria
Sifa ya ugonjwa wa uozo bakteria wa shina la mahindi ni kubadilika rangi kwa majani, kifuko cha jani, na vifundo vya shina. Ugonjwa huu hatimae huenea kwa haraka kwenye shina na kusambaa hadi kwenye majani mengine. Kadri tishu zinapoanza kuoza, harufu mbaya inaweza kugundulika, na sehemu ya juu ya mmea inaweza kuondolewa/kutenganishwa kirahisi kutoka kwenye sehemu nyingine ya mmea. Shina huoza kabisa na mara nyingine sehemu ya juu huanguka. Ukataji wa shina kwa urefu unaonyesha kubadilika rangi ndani na kuoza kwa hali ya utelezi kunakojikita zaidi kwenye pingili. Kwa kuwa bakteria hawaenei kwa mimea mingine, mimea iliyoathirika hupatikana ikitawanyika shambani. Hata hivyo, kuna ripoti za kuenea kwa ugonjwa huu kutoka mmea hadi mmea kupitia wadudu wachache wanaobeba vimelea. Ugonjwa huonekana kwenye mahindi wakati mvua nzito za vipindi zinapofuatiwa na joto kali na unyevunyevu mwingi.
Kwa sasa, hakuna chaguo za kudhibiti wa kibaiolojia zinazopatikana dhidi ya bakteria hawa. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa unafahami mbinu yoyote ya kibaiolojia inayoweza kutumika dhidi ya bakteria hawa.
Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibaiolojia ikiwa yanapatikana. Inashauriwa kuongeza klorini kwenye maji ya umwagiliaji au kutia unga wa kuondoa madoa (bleach) kwa kiwango cha 33% klorini kwa 10 kg/ha kabla ya hatua ya kutoa maua.Mchanganyiko wa copper oxychloride unaweza pia kutumika kwa ufanisi dhidi ya ugonjwa huu. Mwishowe, kuongeza 80 kg/ha ya mbolea ya MOP kwa kuigawanya mara mbili hupunguza ukali wa dalili za ugonjwa.
Dalili za ugonjwa huu husababishwa na bakteria anayefahamika kitaalamu kama Erwinia chrysanthemi ambao msimu wote wa baridi huishi tu kwenye mabaki ya shina yaliyo juu ya uso wa ardhi, lakini hawawezi kuishi kwa zaidi ya mwaka mmoja hapo. Hakuna ushahidi wa kuthibitisha bakteria hawa husambazwa kupitia mbegu. Ugonjwa huu hustawi kwenye joto la 32-35°C na unyevu anga wa juu. Mvua za mara kwa mara na umwagiliaji wa kunyunyuzia husababisha majani kuwa na maji maji kwa muda mrefu na mkusanyiko wa maji kwenye shada. Kadiri maji maji haya yanavyopata joto, yanaweza kuharibu tishu za mmea, na kutoa nafasi kwa maambukizi kutokea. Mimea inayokumbwa na joto kali au mafuriko, mwanzoni inaweza kuonyesha dalili za ugonjwa karibu na kitako cha mmea. Inadhaniwa kuwa maji ya umwagiliaji ni chanzo kikuu cha vimelea. Ingawa ugonjwa unaweza kuenea kwenye mmea na kuathiri vifundo vingine, bakteria hawa kwa kawaida hawasambai hadi kwenye mimea iliyo jirani isipokuwa kama wanabebwa na wadudu wasambazaji wa vimelea.