Clavibacter michiganensis
Bakteria
Dalili kuu kwenye majani ni majeraha ya kahawia yaliyorefuka, yenye kingo zisizo na umbo maalumu zinazoenda sambamba na mishipa ya majani. Kadri muda unavyoenda, majeraha haya yanaweza kusababisha mabaka ya majani, na kuua sehemu kubwa ya shada la majani (kanopi) na kusababisha mimea iwe katika hatari ya kuoza mabua/mashina. Madoa (mabaka) meusi yenye majimaji hujitokeza kwenye majeraha hayo. Mara nyingi, tishu za kwenye kingo za majani hufa. Sehemu zinazong'aa za ute mkavu wa bakteria mara nyingi huonekana kwenye majeraha. Katika mimea ambayo mashina yake yana maambukizi, vifungu vya mishipa yenye rangi ya machungwa vinaweza kuonekana kwenye mashina hayo. Ikiwa maambukizi hutokea katika hatua ya miche, basi mashambulizi hayo husababisha mabaka kwenye mimea michanga, ikiambatana na kunyauka na kufa kwa miche katika baadhi ya maeneo.
Kwa sasa hakuna udhibiti wa kibaiolojia dhidi ya bekteria wanaoneza ugonjwa huu. Tafadhali tujulishe ikiwa unafahamu njia yoyote. Hatua muafaka ya udhibiti kwa sasa ni kinga pekee.
Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kinga pamoja na tiba za kibaiolojia ikiwa zinapatikana. Kwa sasa, hakuna udhibiti kwa njia ya kemikali dhidi ya baketria hawa. Tafadhali tujulishe ikiwa unafahamu njia yoyote ya udhibiti wa kikemikali. Njia muafaka ya kudhibiti tatizo hili ni kinga pekee.
Dalili hizi husababishwa na bakteria anayefahamika kitaalamu kama Clavibacter michiganensis, ambao huendelea kuishi msimu wote wa baridi kwenye mabaki ya mimea iliyoathirika au mabaki ya mimea wenyeji inayoweza kuhifadhi vimelea, ikiwa ni pamoja na nyasi za kijani za mkia wa mbweha (mmea jamii ya shayiri), mimea jamii ya uwele, na ile ya jamii ya mtama. Kutoka kwenye tishu hizi zilizoathirika, bakteria husafirishwa hadi kwenye mimea inayokua hususani kwa njia ya rasharasha za mvua, matone ya maji ya kumwagilia kwa kunyunyuzia ambayo husafirishwa na upepo au. Ugonjwa wa Mnyauko wa Goss huathiri zaidi majani yaliyo na maheraha, kwa mfano, yaliyojeruhiwa kwa mvua ya mawe, kupigwa na mchanga, au dhoruba kali. Ugonjwa huu huenea ndani ya mmea baada ya maambukizi ya majani, na kisha unaweza kuambukizwa kutoka mmea mmoja hadi mwingine. Ukuaji wa ugonjwa huu hustawishwa zaidi na hali ya joto linalozidi 25 °C. Dalili zinakuwa wazi zaidi baada ya mahindi kutoa ndevu, na huongezeka ukali wake baada ya hatua hiyo. Ugonjwa huu huchochewa zaidi kwa kupanda aina ya mbegu chotara zilizo kwenye hatari zaidi ya kuathirika, kupunguza kulima, na kilimo cha mimea ya aina moja kwa muda mrefu.