Mpunga

Baka Bakteria la Suke

Burkholderia glumae

Bakteria

Kwa Ufupi

  • Kubadilika kwa rangi ya punje kuwa kahawia nyepesi hadi kahawia ya kati.
  • Baadaye, punje zinaweza kugeuka kijivu, nyeusi au pinki, kutoka kwa bakteria wengine au fangasi.
  • Suke hubaki wima.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Mpunga

Dalili

Katika mashamba, ugonjwa huu hutokea katika mifumo ya mduara. Makundi madogo ya masuke hayakui vizuri wakati wa kujaza punje na suke hubaki wima badala ya kuinama chini na uzito wa punje. Punje zilizoambukizwa zinaweza kusambaa kwa usawa kwenye suke. Sehemu ya chini ya shina lenye suke liliyoambukizwa inabaki kijani. Bakteria huambukiza punje zinazokua katika hatua ya maua na kusababisha punje kuharibika au kuoza wakati wa kujaza punje baada ya uchavushaji. Punje hubadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia nyepesi hadi kahawia ya kati ya theluthi ya chini hadi nusu ya ganda/punje. Punje hizi zinaweza baadaye kugeuka rangi ya kijivu, nyeusi au pinki wakati bakteria wengine au fangasi husitawi kwenye ganda/punje.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Samahani, hatujui matibabu yoyote ya kibiolojia dhidi ya Burkholderia glumae. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa unajua kitu ambacho kinaweza kusaidia kupambana na ugonjwa huu. Tunatarajia kusikia kutoka kwako.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Samahani, hatujui matibabu yoyote ya kemikali dhidi ya Burkholderia glumae. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa unajua kitu ambacho kinaweza kusaidia kupambana na ugonjwa huu. Tunatarajia kusikia kutoka kwako.

Ni nini kilisababisha?

Baka Bakteria la Suke huenezwa kupitia mbegu. Kuenea kwa ugonjwa huu kunategemea joto. Baka Bakteria la Suke hukua wakati wa joto na ukame katika hatua za baadaye za ukuaji wa mmea. Maambukizi huongezeka wakati halijoto ya mchana ni zaidi ya 32°C na halijoto ya usiku hubakia karibu 25°C au zaidi. Viwango vya juu vya naitrojeni pia huchangia ukuaji wa ugonjwa. Mpunga uliopandwa mapema wakati wa majira ya kuchipua huwa na uharibifu mdogo kutokana na Baka Bakteria la Suke kwa sababu ya halijoto ya baridi wakat kuchanua na kujaza punje.


Hatua za Kuzuia

  • Safisha shamba lako vizuri kutokana na mabaki ya mimea ya mavuno yaliyopita.
  • Panda mbegu zilizoidhinishwa tu, zisizo na magonjwa.
  • Chagua aina ya mpunga wenye ukinzani kiasi ikiwa inapatikana.
  • Panda mazao mapema katika majira ya kuchipua.
  • Dhibiti programu yako ya uwekaji mbolea na usizidishe kipimo kilichopendekezwa, hasa mbolea ya naitrojeni.
  • Epuka kumwagilia kupita kiasi.
  • Fuatilia mazao mara kwa mara na uangalie mimea yenye magonjwa.
  • Zingatia mzunguko wa mazao na mazao yasiyo ya shambuliwa, kama vile mikunde.

Pakua Plantix