Soya

Baka Bakteria la Soya

Pseudomonas savastanoi pv. glycinea

Bakteria

Kwa Ufupi

  • Madoa madogo ya manjano hadi kahawia kwenye majani.
  • Baadaye hugeuka kahawia nyeusi, yasiyo na mpangilio au yenye pembe.
  • Halo ya kijani-manjano.
  • Vidonda vinaonekana pia kwenye maganda.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Soya

Dalili

Maambukizi ya mapema katika msimu yanajulikana kwa madoa ya kahawia kwenye kingo za kotiledon. Mimea michanga inaweza kudumaa na kufa ikiwa sehemu ya ukuaji itaathiriwa. Mimea iliyoambukizwa baadaye katika msimu huota madoa madogo ya manjano hadi kahawia kwenye majani. Majani machanga kwa kawaida huathirika zaidi kuliko yale ya zamani na dalili zinapatikana hasa katikati hadi juu ya taji/mwavuli. Baada ya muda, kadri madoa yanavyo ungana, hubadilika kuwa kahawia nyeusi, vidonda visivyo na mpangilio au vyenye pembe vya ukubwa tofauti. "Halo" ya kijani-manjano huonekana karibu na ukingo wa tishu zilizo lowa maji ambazo huzunguka vidonda. Sehemu ya katikati ya kidonda hukauka polepole na mwishowe huanguka, na kufanya majani kuonekana yame chakaa. Ikiwa maambukizi yatatokea wakati wa hatua ya kuunda maganda, vidonda vinaweza pia kutokea kwenye maganda, na kuyapa mwonekano uliosinyaa na kubadilika rangi. Ingawa, mbegu kwa kawaida hazionyeshi dalili.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Dawa za kuua kuvu za shaba zinapendekezwa kwa ajili ya udhibiti wa baka bakteria kwenye soya. Ili matibabu yawe na ufanisi kamili yafanyike mapema katika mzunguko wa ugonjwa ili kuwa na ufanisi, yaani, wakati dalili zinapogunduliwa kwa mara ya kwanza.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Dawa za kuvu za shaba zinaweza kutumika kudhibiti baka bakteria la soya lakini zinahitaji kutumika mapema katika mzunguko wa ugonjwa ili kuwa na ufanisi. Hata hivyo, inashauriwa kufuata kanuni jumuishi za usimamizi wa wadudu kwani dawa za kuua kuvu mara nyingi hazifanyi kazi dhidi ya vimelea hivi.

Ni nini kilisababisha?

Baka bakteria husababishwa na bakteria Pseudomonas savastanoi. Ni ugonjwa unaoenezwa na mbegu ambao pia husalia shambani kwa msimu wote wa baridi kwenye mabaki ya mimea. Maambukizi ya mapema katika hatua ya miche kawaida ni ishara ya mbegu zilizo na vimelea. Kwa mimea ya zamani, maambukizi ya awali hutokea wakati bakteria walio lala wakienezwa kupitia upepo au matone ya maji kutoka kwenye mabaki ya mimea hadi kwenye majani ya chini. Uso wa jani ulio lowana utachochea maendeleo ya vimelea, ambavyo wakati fulani vitaingia kwenye tishu kupitia majeraha au vitundu vya majani. Mvua na upepo pia vita chochea kuenea kwa upili ndani ya mmea au kati ya mimea. Ugonjwa huu huchagizwa na baridi (20-25 °C), hali ya hewa ya mvua na upepo (dhoruba ya mvua) na kupunguzwa na hali ya hewa ya joto na kavu.


Hatua za Kuzuia

  • Chagua aina zinazostahimili ugonjwa.
  • Usifanye kazi shambani wakati mimea ina unyevu ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa.
  • Changanya mabaki ya mazao kwenye udongo kwa kulima baada ya kuvuna ili kupunguza kiwango cha maambukizi msimu ujao.
  • Panga mzunguko wa mazao na mimea isiyoshambuliwa kama vile mahindi, ngano na mazao mengine yasiyo ya kunde.

Pakua Plantix