Ralstonia solanacearum
Bakteria
Majani machanga zaidi huanza kunyauka wakati wa joto zaidi mchana na kwa kiasi fulani hupona pale hali ya joto inapopungua. Chini ya hali nzuri, kunyauka kunaweza kuathiri mmea wote moja kwa moja. Majani yaliyonyauka hubaki na rangi yake ya kijani kibichi na kubaki yamejishikiza kwenye shina. Mizizi na sehemu ya chini ya shina huonyesha rangi ya kahawia iliyokolea. Mizizi iliyovamiwa inaweza kuoza kutokana na maambukizi ya upili ya bakteria. Wakati wa kukatwa, shina linaweza kuvuja majimaji mithili ya maziwa yenye rangi nyeupe au njano.
Matumizi ya mboji kwa wingi (mbolea ya kijani) kutoka kwa mimea ya familia ya cruciferous kwenye udongo (biofumigation) inaweza kusaidia kudhibiti vimelea hao. Mimea au sehemu za mmea zinaweza kusagwa au kukatwa katwa kabla ya kuchimbiwa kwenye udongo, ama kwa mitambo au kwa mkono. Kemikali inayotokana na mimea iitwayo Thymol ina matokeo sawa. Bakteria mshindani ambae hutawala mifumo ya mizizi ya mimea aina ya solanaceous pia anafaa.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Kwa sababu ya asili ya vimelea hao kusambazwa kwa njia ya udongo, matibabu ya kikemikali ya ugonjwa yanaweza kutofaa, kuwa na kiwango kidogo cha ufanisi au kukosa kabisa ufanisi.
Bakteria anaweza kuishi kwa muda mrefu kwenye udongo, anaweza kuishi kwenye uchafu wa mimea au kwenye mimea mingine ambayo ni mwenyeji mbadala. Huingia kwenye mmea kupitia majeraha katika mfumo wa mizizi wakati wa kuibuka kwa mizizi ya pembeni. Joto la juu (kutoka 30 ° C hadi 35 ° C), unyevu wa juu na unyevu wa udongo, na pH (yaani kiwango cha tindikali na alikali kwenye udongo) ya udongo wa alkali hupelekea maendeleo ya ugonjwa. Udongo mzito ambao unaweza kuhifadhi unyevu wa udongo kwa muda mrefu ni hatari sana. Wenyeji wakuu mbadala wa Ralstonia solanacearum ni pamoja na nyanya, tumbaku, migomba na ndizi.