Muwa

Baka-jani Bakteria la Miwa

Acidovorax avenae

Bakteria

Kwa Ufupi

  • Michirizi ya kijani yenye maji maji kando ya mshipa mkuu wa katikati na kwenye kitako cha jani.
  • Mistari yenye rangi nyekundu huenea kwenye jani zima.
  • Kunyauka na kuoza kwa majani.
  • Kupungua kwa mfumo wa mizizi.
  • Ukuaji uliodumaa.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Muwa

Dalili

Ugonjwa huu hutokea zaidi kwenye majani machanga na ya umri wa kati. Michirizi mirefu, myembamba, inayofanana ya rangi ya kijani na yenye maji maji hutokea kwanza karibu na mshipa mkuu wa katikati na kitako cha ubapa wa majani. Katika hatua za baadaye za ugonjwa huo, michirizi huenea kwenye jani lote, huungana na kuwa baka la kwanza lenye rangi nyekundu-nyepesi na kisha rangi nyekundu-nyeusi (kufa kwa tishu). Majani hunyauka, kuoza na kutoa harufu mbaya. Uozo unapoendelea ndani ya shina, mashimo makubwa huundwa ndani ya pingili. Katika hatua za baadaye za ugonjwa huo, ncha na vishada vya maua mara nyingi huvunjika na kuanguka chini, dalili hii inaitwa kuoza kwa juu.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Kwa bahati mbaya, hakuna mbinu bora za udhibiti wa kibiolojia zinazopatikana kwa wakati huu.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Ili kuzuia maambukizi ya awali, matibabu ya mbegu kwa kutumia dawa inayofaa kwa muda wa dakika 15 hadi 20 yanaweza kufanywa.

Ni nini kilisababisha?

Bakteria hupendelea unyevu wa juu na joto la juu. Maambukizi ya awali hufanyika kupitia udongo na vipandikizi vyenye magonjwa, wakati maambukizi ya upili hutokea kupitia hewa, matone ya mvua na udongo.


Hatua za Kuzuia

  • Panda aina sugu.
  • Kusanya vipandikizi vyenye afya kutoka kwenye kitalu cha mbegu.
  • Tekeleza mzunguko mpana wa mazao na mazao ya mboji ya kijani.
  • Boresha mfumo wako wa mifereji ya maji ili kupunguza matukio ya ugonjwa huo.
  • Weka mbolea zenye naitrojeni kiasi.

Pakua Plantix