Pseudomonas savastanoi pv. savastanoi
Bakteria
Dalili kuu inayoonekana ya ugonjwa huu ni kuonekana kwa mafungo kwenye vijitawi, matawi, shina na mizizi wakati masika na majira ya joto. Kwa kawaida hutokea kwenye matawi lakini si mara zote kwenye vifundo vya majani au shina la matunda. Uharibifu huu wa gome unaweza kufikia sentimita kadhaa kwa kipenyo na mara chache huweza kutokea kwenye majani au machipukizi. Kufa kwa shina ni kawaida, kwani uvimbe huo huzuia usafirishaji wa virutubisho na maji kwenda kwenye tishu. Kwa ujumla, miti iliyoambukizwa huwa dhaifu na kupungua ukuaji. Mafundo yanapokua, hujizungushakwenye tawi na kuua matawi yaliyoathiriwa, na hivyo kusababisha kupungua kwa ukubwa na ubora wa matunda au kufa kwa mti iwapo bustani ni mpya.
Tumia dawa kuzuia bakteria mara mbili kwa mwaka (masika na majira ya kuchipua) na bidhaa za asili, zenye shaba hupunguza sana uundwaji wa mafundo kwenye miti. Vidonda vya kupogoa vinapaswa pia kutibiwa kwa dawa za kuua bakteria zenye shaba (mchanganyiko wa Bordeaux kwa mfano) ili kupunguza uwezekano wa kuambukizwa. Baadhi ya bidhaa zenye sulfate ya shaba pia zinaruhusiwa katika kilimo hai kilichoidhinishwa.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Ni vigumu sana kudhibiti vimelea hivi. Matumizi mara mbili ya dawa za kuzuia bakteria kwa mwaka (masika na kipindi cha kuchipua) zenye shaba (pamoja na mancozeb) hupunguza sana matukio ya ugonjwa huu katika bustani. Vidonda vya kupogoa vinapaswa pia kutibiwa kwa dawa za kuua bakteria zenye shaba ili kupunguza uwezekano wa kuambukiza. Miti iliyovunwa kwa mitambo inapaswa kutibiwa mara baada ya kuvuna.
Dalili husababishwa na aina ya bakteria wa spishi Pseudomonas savastanoi. Vimelea hawa hustawi zaidi kwenye gome kuliko kwenye majani ya mizeituni. Ukali wa maambukizi hutofautiana kutoka kwa aina mbalimbali, lakini miti michanga ya mizeituni kwa ujumla huathirika zaidi kuliko iliyokamaa. Bakteria hao huishi kwenye mafundo na hutolewa nje kama sehemu ya majimaji ya bakteria wakati mvua inaponyesha. Huenea kwa mimea yenye afya kwa njia ya matone ya mvua au kwa mitambo mwaka mzima. Makovu ya majani, nyufa za gome, majeraha ya kupogoa au kuvuna husaidia kusambaa kwake. Uharibifu wa theluji wakati wa msimu wa baridi ni shida sana kwani kawaida huambatana na siku za mvua, na hivyo kuunda hali nzuri kwa magonjwa ya mlipuko. Uvimbe huonekana ndani ya siku 10 hadi miezi kadhaa baada ya kuambukizwa, kwa mara moja au mfululizo.