Liberibacter asiaticus
Bakteria
Kwa kawaida dalili ya kwanza ni kuonekana kwa rangi ya njano katika sehemu zinazo chipua kwenye mti, hivyo jina moja la maarufu la ugonjwa huo ni huanglongbing ("ugonjwa wa dragoni wa njano"). Polepole majani huanza kubadilika na kuwa ya manjano iliyo fifia na kuonyesha mabaka yaliyosambaa ambayo yanaweza kufanana na upungufu madini ya zinki au manganizi. Njia ya kawaida ya kutofautisha matatizo haya ni kwamba dalili za upungufu huu ( wa zinki na manganizi) huwa na mlingano kando ya mshipa wa jani, wakati dalili za ugonjwa huu hazilingani. Miti iliyoathirika zaidi huonyesha ukuaji uliodumaa, kudondoka kwa majani mapema na kufa kwa matawi. Miti inaweza kutoa maua mengi nje ya msimu, maua ambayo baadaye huanguka na pia hutoa matunda madogo yasiyo ya kawaida, yenye ganda nene, lenye rangi iliyokwajuka/fifia ambayo hubakia kuwa ya rangi kijani sehemu ya chini.
Samahani, hatufahamu matibabu yoyote ya kibaiyolojia dhidi ya ugonjwa huu. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa unajua kitu chochote ambacho kinaweza kusaidia kupambana na ugonjwa huu. Tunatarajia kusikia zaidi kutoka kwako.
Daima zingatia mbinu jumuishi pamoja na hatua za kinga na matibabu ya kibaiolojia ikiwa yanapatikana. Matumizi sahihi ya viuatilifu yameleta matokeo mazuri katika kudhibiti vijidudu vya chawa wa mimea na hivyo kupunguza kuenea kwa ugonjwa. Sindano ya vijiuasumu (antibiotiki) ya tetrasaiklini, (maarufu kama dawa za rangi mbili) kwenye shina la miti inaweza kusababisha ahueni ya kiasi lakini inabidi irudiwe mara kwa mara ili kuonyesha matokeo mazuri. Tetrasaiklini ni sumu kwa mimea na inaweza kuwa na madhara kwa mazingira. Kwa sababu hizi, matumizi yake yamepungua katika miaka ya hivi karibuni.
Dalili za ugonjwa wa rangi ya kijani (huanglongbing - HLB) husababishwa na bakteria aitwae Candidatus Liberibacter asiaticus. Ugonjwa huu husambazwa kwa njia endelevu na chawa wa mimea (psyllid) ambavyo wapo kila mahali kwenye mashamba ya machungwa, Diaphorina citri na Trioza erytreae. Ugonjwa unaweza kupatikana kupitia tunutu pamoja na wadudu kamili, ambao wanaweza kudumisha na kusambaza ugonjwa huo katika kipindi chote cha maisha yao cha miezi 3 hadi 4. Ugonjwa wa rangi ya kijani ni ugonjwa unaotokea hatua kwa hatua na una kipindi cha kuatamiza/kuatamia cha miezi mitatu hadi miaka kadhaa kabla ya dalili kuonekana. Ugonjwa huu pia unaweza kusambazwa kupitia upandikizaji/kuunganisha mimea, ingawa kwa viwango tofauti vya usambazaji. Uambukizaji kupitia mbegu pia unawezekana. Magonjwa au matatizo mengine pia yanaweza kuonyesha madoa ya majani kama hayo. Inashauriwa kutuma sampuli za tishu kwa uchunguzi maabara ili kuthibitisha chanzo cha ugonjwa.