Mti wa jamii ya mchungwa

Kikwachu cha Michungwa

Xanthomonas axonopodis pv. citri

Bakteria

Kwa Ufupi

  • Kwenye majani kuna mashimo yaliyo mithili ya dutu yenye rangi ya kutu-kahawia yakiwa yamezungukwa na mduara wenye angavu wa manjano.
  • Baadaye vidonda vyenye rangi ya kahawaia isiyokolea au ya kijivu katikati, na kingo za kahawia zenye hali ya mafuta na kulowana maji.
  • Dalili kama hizo pia huonekana kwenye matunda na vijiti vya matawi.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Mti wa jamii ya mchungwa

Dalili

Miti inaweza kuathiriwa katika hatua zote za ukuaji wake, na dalili zinaweza kutokea kwenye majani, matunda, au vijiti vya matawi. Vidonda vidogo sana vilivyo mithili ya sponji, vilivyoinuka kiasi hutokea kwanza kwenye pande zote mbili za majani yaliyoambukizwa karibuni. Kadri vinapokomaa, vidonda hivi hugeuka kuwa makovu mithili ya dutu (uvimbe) yenye rangi ya kutu-kahawia ambayo imezungukwa na mduara wenye mwanga angavu wa manjano. Hatimaye, vidonda hivi hupasuka, na kutoa vitu vilivyomo, na kutengeneza kidonda (jeraha) lenye sehemu ya katikati yenye rangi ya kahawia iliyofifia au kijivu, pamoja na ukingo wa kahawia uliolowana maji na kuwa mithili ya mafuta. Wakati mwingine, sehemu ya katikati ya kikwachu cha zamani hudondoka, na kusababisha athari au alama ya shimo la risasi. Dalili kama hizo zinaweza kuonekana kwenye matunda na vitawi, ambako vikwachu vinaweza kufikia ukubwa wa kadiri. Sehemu ya katikati ya kidonda huinuka, na kuwa na mwonekano wa kovu au gamba. Matokeo yake ni kupukutika kwa majani na kudondoka kwa matunda kabla ya kukomaa, na vitawi vinaweza kufa kutokana na tishu za mishipa kuzungukwa na vidonda. Matunda yanayofikia kukomaa huwa hayana soko.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Kwa bahati mbaya, hakuna mbinu za udhibiti wa kibaiolojia zenye ufanisi ambazo zinapatikana kwa wakati huu.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kinga pamoja na matibabu ya kibaiolojia, ikiwa yanapatikana. Kwa bahati mbaya, hakuna njia yenye ufanisi ya kudhibiti kikwachu cha machungwa mara ugonjwa huu unapokuwa umebainika. Hatua za kinga kama vile kuondoa na kuharibu miti iliyoanguka ni mbinu muhimu ili kupunguza athari za ugonjwa. Udhibiti wa mlusina wa machungwa, pia inaweza kuwa njia ya kudhibiti uharibifu. Dawa za kuua kuvu au bakteria zinazotokana na shaba zinaweza kutoa kizuizi dhidi ya maambukizi, lakini hazitapunguza maambukizi ambayo tayari yapo.

Ni nini kilisababisha?

Kikwachu cha jamii ya machungwa ni ugonjwa hatari na unaoambukiza sana aina za machungwa ya kibiashara na mimea ya jamii hiyo. Ugonjwa huu husababishwa na bakteria aitwae Xanthomonas citri, ambao wanaweza kuishi kwa zaidi ya miezi 10 katika majeraha ya zamani kwenye matunda, majani, na mashina. Bakteria huingia kwenye tishu za mmea kupitia vidonda au matundu ya asili kwenye uso wa jani na hukua humo kwa kuenea kwenye mfumo mzima wa mmea. Mashimo yanayojitokeza kwenye majani na tishu zingine yanakuwa na bakteria, ambao hutolewa wakati wa majani yanapolowana na kusambaa kupitia matone ya mvua au mifumo ya umwagiliaji wa juu kwa umbali mfupi. Hali zinazowezesha ugonjwa ni unyevu wa juu, hali ya hewa ya joto (20 hadi 30 °C), na mvua, hususani ikiwa na upepo mkali. Mlusina wa Machungwa (Citrus psyllids), kidomozi, ndege, pamoja na zana na vifaa vilivyoambukizwa, vinaweza pia kusambaza bakteria kati ya miti au mashamba. Hatimaye, usafirishaji wa mimea au sehemu za mimea zilizoambukizwa kama vile miti ya kitalu au vifaa vya uzalishaji ni tatizo jingine kubwa.


Hatua za Kuzuia

  • Angalia kanuni za karantini katika eneo lako.
  • Chagua aina za machungwa zinazostahimili zaidi ugonjwa.
  • Hakikisha mbegu na miche yenye afya, ikiwezekana kutoka vyanzo vilivyothibitishwa.
  • Fuatilia miti ili kubaini dalili za uwepo wa ugonjwa.
  • Punguza sehemu za miti zilizoambukizwa wakati wa msimu wa ukame.
  • Takasa (Safisha kwa dawa za kuua vimelea) zana na vifaa vya kilimo kila unavyomaliza kutumia sehemu moja ili kuepusha kueneza ugonjwa kutoka sehemu moja hadi nyingine.
  • Epuka kufanya kazi shambani wakati majani yakiwa yamelowana.
  • Safisha vizuri viatu na nguo ulizovaa wakati wa kufanya kazi kwenye shamba moja kabla hujaenda kufanya nazo kazi kwenye shamba lingine.
  • Haribu miti iliyoathiriwa vibaya ili kuzuia kuambukiza miti yenye afya iliyo jirani.
  • Ondoa majani, matunda, na matawi yaliyodondoka chini na yaharibu.
  • Tumia vizuizi vya upepo kati ya shamba na shamba ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa.

Pakua Plantix