Mpunga

Michirizi-bakteria ya Jani

Xanthomonas oryzae pv. oryzicola

Bakteria

Kwa Ufupi

  • Vidonda vilivyo jipanga kwa mstari kwenye majani vyenye rangi ya kijani kilichokolea, baadaye kahawia hadi manjano-kijivu.
  • Majani yote yanaweza kugeuka kahawia.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Mpunga

Dalili

Katika hatua ya awali ya maambukizi, majani yanaonyesha michirizi ya kijani-kibichi na madoa yaliyotota maji kwenye majani yaliyoambukizwa. Vidonda hivi huongezeka kwa idadi na kuwa na rangi ya njano-machungwa hadi kahawia. Vidonda vinaweza kuonyesha matone ya rangi ya kahawia yenye vioevu/majimaji/utomvu wa bakteria. Baadaye, dalili zinazoonekana za kuambukizwa na michirizi-bakteria ya jani zinafanana sana na zile za Baka-jani, lakini vidonda vinavyosababishwa na michirizi-bakteria ya jani vina vimenyooka zaidi na kingo hazina mawimbi kama kingo za majani yaliyoambukizwa na Baka-jani.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Samahani, hatujui matibabu yoyote mbadala dhidi ya Xanthomonas oryzae pv. oryzicola. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa unajua kitu ambacho kinaweza kusaidia kupambana na ugonjwa huu. Tunatarajia kusikia kutoka kwako.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi yenye hatua za kinga na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Katika kesi ya maambukizi makali, tumia dawa za kuvu zenye msingi wa shaba wakati wa kutokea kwa masuke ili kudhibiti ugonjwa kwa ufanisi. Dawa za kuvu zenye shaba hazipaswi kutumiwa katika hatua za awali, zitumike tu kwenye hatua za baada ya kutokea maua.

Ni nini kilisababisha?

Bakteria huenezwa kwa maji ya umwagiliaji na maambukizi yanahusishwa na mvua, unyevu wa juu na joto la juu. Ugonjwa haukui katika hali ya baridi na kavu. Bakteria huingia kwenye jani kupitia stomata na majeraha na kuzaliana ndani. Kulingana na hali ya unyevu wakati wa usiku, utomvu wa bakteria huundwa kwenye uso wa jani.


Hatua za Kuzuia

  • Panda miche yenye afya, sugu.
  • Weka mashamba katika hali ya usafi na uondoe magugu.
  • Lima kwa kufukia chini mabua ya mpunga, nyasi, Machipukizi ya mpunga uliovunwa, na miche ya kujiotea yenyewe.
  • Hakikisha matumizi bora ya virutubisho, haswa naitrojeni.
  • Boresha mifumo ya kupitisha maji kwenye mashamba na vitalu.
  • Kausha shamba katika kipindi cha kupumzisha ili kuua bakteria kwenye udongo na mabaki.
  • Ondoa maji shambani wakati wa mafuriko makubwa.
  • Panda mbegu katika vipindi vya baridi ili vimelea visiweze kukua.

Pakua Plantix