Mpunga

Bakajani bakteria wa mpunga

Xanthomonas oryzae pv. oryzae

Bakteria

Kwa Ufupi

  • Michirizi ya kijivu inayo karibia kijani kwenye majani.
  • Majani kuwa ya njano na kunyauka.
  • Matone ya utomvu wenye rangi ya maziwa hutoka kwenye majani.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Mpunga

Dalili

Kwenye miche, majani yaliyoambukizwa kwanza hugeuka kuwa ya njano na kuwa na rangi ya kijivu-kijani na baadaye kunyauka na kufa. Kwenye mimea iliyokomaa, ugonjwa huanza kutokea hasa kipindi cha kuchipua kwa mashina hadi kuchanua. Kijani nyepesi hadi kijivu-kijani, michirizi yenye maji maji huonekana kwanza kwenye majani. Michirizi inapounganika, huunda vidonda vikubwa vya manjano na kingo zisizo sawa. Majani huwa ya manjano na polepole hunyauka na kufa. Katika hatua ya mwisho ya maambukizi, matone ya utomvu wa bakteria yenye rangi ya maziwa yanaweza kuonekana yakitoka kwenye majani. Matone haya yanaweza kukauka baadaye na kuacha ukoko mweupe. Sifa hii inaweza kusaidia kutofautisha ugonjwa huu na uharibifu unaosababishwa na baadhi ya vipekecha shina. Bakajani bakteria wa mpunga ni mojawapo ya magonjwa makubwa zaidi ya mpunga.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Hadi leo, hakuna bidhaa za kibaolojia zinazopatikana kibiashara kudhibiti Bakajani bakteria kwenye mpunga. Uwekaji wa bidhaa zenye madini ya shaba unaweza kusaidia kupunguza dalili lakini hautadhibiti ugonjwa huo.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kinga na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Ili kukabiliana na Bakajani bakteria wa mpunga, unashauriwa kutibu mbegu kwa madawa ya antibaiotiki yaliyoidhinishwa pamoja na copper oxychloride au copper sulphate. Matumizi ya antibaiotiki yamewekewa vikwazo vikali katika baadhi ya nchi, kwa hiyo tafadhali zingatia hatua zinazotumika katika nchi yako.

Ni nini kilisababisha?

Ugonjwa huu husababishwa na bakteria ajulikanae kama Xanthomonas oryzae pv. oryzae, ambae huweza kuishi kwenye magugu ya nyasi au mabua ya mimea iliyoambukizwa. Vimelea hivi huenezwa na upepo na mvua au maji ya umwagiliaji. Hivyo, matukio ya magonjwa na ukali huongezeka wakati wa hali mbaya ya hewa (mvua ya mara kwa mara, upepo), unyevu wa juu (zaidi ya 70%) na hali ya joto la (25 ° C hadi 34 ° C). Matumizi kwa wingi ya mbolea zenye naitrojeni au upandaji wa karibu pia husababisha ugonjwa huo, hasa katika aina za mbegu zisizo na ukinzani wa magonjwa. Kadri ugonjwa unavyo tokea mapema, ndivyo upotevu wa mavuno huongezeka. Ikiwa mimea imeambukizwa wakati wa kuanza kutengeneza masuke, mavuno hayawezi kuathiriwa lakini sehemu kubwa ya punje za mchele huvunjika. Ugonjwa huu hutokea kote katika mazingira ya kitropiki na baridi, hasa katika maeneo ya umwagiliaji na nyanda za chini zinazo tumia maji ya mvua.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia mbegu zenye afya tu, ikiwezekana kutoka kwenye chanzo kilichoidhinishwa.
  • Panda aina za mpunga zinazostahimili ugonjwa huu, hii ndiyo njia bora na ya kuaminika ya kudhibiti ugonjwa huu (na ni nafuu zaidi).
  • Shika mche kwa uangalifu wakati wa kupandikiza.
  • Hakikisha kuna mfumo mzuri wa kuingiza na kutoa maji kwenye shamba na kitalu ili kuzuia kuhamisha vimelea vya ugonjwa kutoka shamba/kitalu kimoja kwenda kingine.
  • Punguza matumizi ya mbolea zenye naitrojeni ili kuepuka kuzidi kiwango na weka kwa awamu kadhaa ndani msimu.
  • Weka dozi ya ziada ya potashi pamoja na dozi ya mwisho ya naitrojeni wakati hali ya hewa ni nzuri.
  • Epuka matumizi ya naitrojeni katika mfumo wa yurea.
  • Haribu na ondoa magugu na mimea ambayo ni mwenyeji mbadala(alternative hosts) kutoka kwenye njia na maeneo yanayozunguka shamba.
  • Lima kwa kufunika chini mabua ya mpunga, majani, mabuu na maotea ambayo huweza kutumika kama mwenyeji wa bakteria.
  • Ruhusu mashamba kukauka kabla ya msimu mwingine kuanza ili kuharibu mawakala wa magonjwa kwenye udongo na mabaki ya mimea au pumzisha shamba.

Pakua Plantix