Stroberi

Doa-jani la Stroberi Lenye Pembe

Xanthomonas fragariae

Bakteria

Kwa Ufupi

  • Madoa yaliyotota maji, yaliyo angavu na yenye pembe upande wa chini wa majani.
  • Baadaye madoa haya huungana na kutengeneza mabaka ya rangi ya kahawia-nyekundu.
  • Ute wa bakteria hutoka kwenye vidonda hivi.
  • Mashina ya matunda hubadilika kuwa meusi na matunda yaliyonyauka.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao
Stroberi

Stroberi

Dalili

Dalili hutofautiana kutegemea na aina ya mmea, hali ya hewa, na wakati wa mwaka. Hapo awali, ugonjwa hutambulika kwa uwepo wa madoa yenye pembe, yaliyotota maji, huku yakiwa na rangi ya kijani kibichi kwenye upande wa chini wa majani. Yakishikiliwa dhidi ya mwanga wa jua, madoa haya huonekana angavu na kupitisha mwanga na kutengenezwa kwa mishipa midogo ya jani. Unyevu unapokuwa mwingi, matone yenye kunata ya ute wa bakteria hutoka kwenye vidonda hivi. Kadri ugonjwa unapoendelea, vidonda hatimaye huonekana kama madoa yasiyo na umbo maalumu, yenye rangi ya kahawia au nyekundu kwenye upande wa juu wa jani. Baadaye madoa haya huungana na kuunda mabaka makubwa yanayotokana na kufa kwa tishu, na kuyafanya majani yawe na mwonekano wa kubabuka. Mashina ya matunda yanaweza kugeuka rangi na kuwa ya hudhurungi-nyeusi na matunda yanaweza kunyauka kwa vile usambazaji wa maji unakuwa umekatika. Hii inaathiri ubora wa matunda na mwonekano wake. Matunda hayatakuwa na sukari nyingi, lakini uendelevu ni kawaida kabisa.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Kupulizia mchanganyiko wa shaba ya kikaboni iliyoidhinishwa inaweza kusaidia kupunguza ugonjwa huo. Matumizi ya mchanganyiko wenye asidi inayotokana na matunda jamii ya machungwa na ile inayotokana na maziwa pia unaweza kusaidia kukinga majani na matunda yanayokua dhidi ya maambukizo mapema msimu.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibaiyojia ikiwa yanapatikana. Madawa yanayotokana na shaba yanaweza kutumika katika joto la chini ili kupunguza maambukizi kutoka kwa mmea hadi mmea kupitia ute unaochiruzika wa bakteria. Hata hivyo, marudio na kipimo vinahitajika kupangiliwa kwa uangalifu, ili mimea isiharibike. Usitumie madawa shaba wakati wa hali ya hewa yenye ukavu na baada ya kuanza kutoka maua. Michanganyiko ya hidroksidi ya shaba inaweza kuwa na ufanisi zaidi kuliko mchanganyiko wa wa sulfate ya shaba. Matumizi ya asidi ya Oxolinic yameonyesha kuwa na matokeo mazuri katika hatua ya vitalu. Mchanganyiko wa Validamycin-A una ufanisi katika hatua ya ulimaji.

Ni nini kilisababisha?

Dalili husababishwa na bakteria Xanthomonas fragariae, ambao wanaweza kuishi msimu wote wa baridi kwenye mabaki ya majani makavu yaliyo chini ya udongo au kwenye majani yaliyofukiwa kwenye udongo. Bakteria hawa wanakuwa sugu sana katika hali mbaya kama vile kukata ukaukaji. Wakati wa majira ya kuchipua, vimelea huanza kukua tena na kuingi kwenye mimea mipya yenye afya, na kusambazwa kutoka mmea mmoja hadi mwingine kwa njia ya matone ya mvua au maji ya umwagiliaji wa kutokea juu. Ute unaotolewa chini ya uso wa jani ni chanzo cha pili cha chanjo. Katika hali zote mbili, bakteria huingia kwenye mmea kupitia vinyweleo (vitundu) vyake vya asili au kupitia majeraha yanayotokana na shughuli za shambani. Vinginevyo, vipandikizi vyenye maambukizi vinaweza kuleta ugonjwa kwenye shamba jipya. Ugonjwa huu unastawi zaidi katika hali ya ubaridi na chepechepe, kwa mfano siku za ubaridi wakati wa mchana na baridi kali wakati wa usiku.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia mbegu zenye afya kutoka kwenye vyanzo vilivyoidhinishwa kwa ajili ya kupanda.
  • Panda aina ya mbegu zilizo sugu dhidi ya magonjwa, ikiwa zinapatikana katika eneo lako.
  • Weka nafasi ya kutosha kati ya mmea na mmea ili kuruhusu mzunguko mzuri wa hewa.
  • Wakati wa kumwagilia, hakikisha ukaukaji wa haraka kwa mimea kwa kumwagilia mapema na epuke umwagiliaji wa maji kutokea juu.
  • Matandazo ya majani yanaweza kusaidia kupunguza umwagikaji wa maji.
  • Punguza usafirishaji wa vifaa vya kilimo na vya kuvunia kutoka sehemu moja hadi nyingine kupitia majani yenye yaliyolowana.
  • Epuka majeraha ya mimea wakati wa kazi ya shamba.
  • Mzunguko wa mazao unapendekezwa.
  • Usipande stroberi kwa kipindi cha miaka 3 inayofuata eneo ambalo pamegunduliwa Doa-jani la Stroberi Lenye Pembe.

Pakua Plantix